Anakwenda Merseyside? Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o anaweza kujiunga na Liverpool.
MCAMEROON, Samuel Eto'o yuko tayari kukamilisha usajili wa ghafla kujiunga na Liverpool.
Mario Balotelli aliwasili Merseyside
jana kujaribu kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 16 kujiunga
Anfield, lakini kama dili litashindikana, nafasi yake itachukuliwa na
Mcameroon.
Inafahamika kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea alipimwa afya na Liverpool akiwa mjini Paris jana ijumaa.
Eto'o mwenye miaka 33 ambaye anaishi mji
mkuu wa Ufaransa, amekubali dili la miezi 12 (mwaka mmoja) kujiunga na
Liverpool na anasubiri kupanda ndege kwenda kusaini mkataba.
Eto’o aliripotiwa kuvutiwa na Everton
kwa siku chache zilizopita, lakini kigezo cha kucheza ligi ya mabingwa
kimemfanya aichague Liverpool.
Picha hii ya Mcameroon huyu alikuwa katika fainali za kombe la Dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil.
0 maoni:
Post a Comment