Mlinzi wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Mats Hummels amefunga pingu za maisha na mpenzi wake wa muda mrefu, Cathy Fischer. Ndoa
ya mshindi huyo wa kombe la dunia ambaye miezi ya karibuni amekuwa
akihusishwa kujiunga na Manchester United alifunwga jana mjini Munich. Hummels mwenye miaka 26 alipigwa picha akiwa na mapambo yenye rangi ya jezi ya Borussia kwenye suti yake maridadi kabisa....
Tuesday, June 16, 2015



Timu
ya taifa ya soka ya Uganda yenye wachezaji wanaocheza soka nyumbani
imeanza maandalizi ya michuano ya mzunguko wa kwanza kufuzu kwa michuano
ya Afrika CHAN itakayofanyika mwakani nchini Rwanda. Uganda inajiandaa kuchuana na Tanzania siku ya Jumamosi mchuano utakaochezwa katika visiwa vya Zanzibar. Kocha
Milutin ‘Micho’ Sredojevic anasema baada ya mchuano wa mwishoni mwa
juma lililopita...


Kiungo
wa zamani wa klabu ya Manchester United, Cleverley mchana wa leo
alifunga pingu za maisha na mchumba wake wa muda mrefu Georgina Dorsett
katika shughuli ya kifahari iliyofanyika huko Claridge.
Ndoa
hiyo ilihudhuriwa na mastaa wengi wa soka akiwemo nahodha wa klabu ya
Manchester United na England Wayne Rooney ambaye pia aliongozana na
mkewe Coleen,...


Mshindi wa mbio za Acacia Tufanikiwe Pamoja Lake Zone Cycle Challenge,
Masunga Duba aliyeinua mikono akishangilia mara baada ya kumaliza mbio
hizo akiwa mbele ya wenzake. Mshindi huyo anatoka mkoa wa Shinyanga.
Makamu wa rais wa Kampuni ya Uchimbaji wa dhahabu ya Acacia, Deo
Mwanyika (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo na Afisa Mkuu wa
Uendeshaji wa kampuni ya Acacia, Mishel Ash,...


Ratiba ya Msimu mpya wa 2015/2016 wa Ligi Kuu England itatolewa Kesho Jumatano Saa 5 Asubuhi. Pamoja
na Ratiba hiyo ya Ligi ya juu England pia zitatolewa Ratiba za Ligi za
chini yake kwa Msimu huo mpya ambao unahusisha jumla ya Timu 92 kwa
Madaraja yake yote. Chelsea ndio Mabingwa wa Ligi Kuu England
walipotwaa Ubingwa wakiwa Pointi 8 mbele ya Timu ya Pili Manchester City
waliofuatiwa...


AC Milan wamemteua Kocha wa zamani wa Serbia Sinisa Mihajlovic baada kumtimua Filippo Inzaghi. Mihajlovic,
ambae ni Beki wa zamani mwenye Miaka 46, amesaini Mkataba wa Miaka
Miwili na kibarua chake cha mwisho kama Kocha kilikuwa huko Sampdoria
ambako aliondoka mwanzoni mwa Mwezi huu. Flippo Inzaghi, mwenye Miaka 41, alikuwa Mchezaji wa zamani wa AC Milan aliyoichezea kuanzia 2001 hadi...


TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars leo imerejea
nchini kutoka Misri ilipokwenda kucheza mechi ya kuwania kufuzu fainali za
Kombe la Mataifa Afrika mwishoni mwa wiki iliyopita na kufungwa mabao 3-0.
Kwa muda mrefu Stars haijapata matokeo mazuri kwenye
mechi za kimataifa hali iliyofanya wachezaji wake kutoka uwanja wa ndege kwa
mafungu huku wengine wakikwepa kuzungumza na vyombo...


Jokate (kushoto) akizungumza
katika mkutano wa jukwaa la sanaa. Katikati ni katibu mkuu wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz), Hassan
Bumbuli na mbunifu mkongwe wa mavazi, Asia Idarous.
Mbunifu mkongwe wa mavazi nchini,
Asia Idarous (kulia) akisisitiza jambo katika mkutano wa jukwaa la
sanaa. Katikati ni Katibu mkuu wa...


Wakala wa Fowadi wa Hoffenheim Roberto Firmino amethibitisha kuwa Mchezaji huyo anahamia England kwa ajili ya Msimu ujao. Roger
Wittmann, ambae anamwakilisha Nyota huyo mpya anaewika kutoka Brazil
mwenye Miaka 23, amekataa kutoboa waziwazi ni Klabu ipi Mchezaji wake
huyo atakwenda ingawa hivi karibuni amehusishwa na kujiunga na
Manchester United. Akiongea na Gazeti la Ujerumani, Bild, Wittmann...


Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto), akiwa na Waziri wa Habari
Vijana Utamaduni na Michezo, Dk.Fenellah Mukangala (kulia) aliyekuwa
mgeni rasmi katika fainali za mashindano ya Mtemvu CUP yaliyofikia
tamati viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam jana. Timu zilizoingia
ingia fainali hiyo ni Miburani Kata ya 15 na Kata ya 14 ambayo iliibuka
kidedea kwa ushindi wa bao 1-0.
Mbunge...


Kiongozi
wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Akifurahia mara baada ya kutua
Bukoba na tayari kuwahutubia wakazi wa mji wa Bukoba leo wakati wa
mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mashujaa/Uhuru Platform Bukoba leo
Jumatatu tarehe 15 june, 2015. Kiongozi huyu ambaye amefuatana na
viongozi wenzake wa juu wa chama hicho, yuko kwenye ziara ya kukitangaza
chama na sera mpya ya azimio...
Subscribe to:
Posts (Atom)