Tuesday, August 5, 2014
8:06 AM
Unknown
8:01 AM
Unknown
Akiongea na Mwaandishi wa Bukobasports.com Mc Jerry kwa jina maarufu hapa Bukoba amesema Bendi hiyo itatua hapa Mjini kwa ajili Burudani ya Nguvu na pia alifafanua kuwa Tangu Bendi hii ianzishwe ni Onesho lao la kwanza hapa Bukoba hivyo anawataka Wakazi kuingia kwa wingi kushuhudia Bendi hiyo ikifanya mambo yake live Jukwaani.
Alisema kuwa bendi nzima ya Mashujaa inatarajiwa kutia timu mjini hapa wakiwa na wanamuziki wake wote ambapo aliwataja baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo kuwa ni pamoja na Chaz Baba.
Alifafanua zaidi kuwa Bendi hii imedhamiria ‘kufunika’ katika onyesho hilo na wamejipanga kufunika bendi zote ambazo zimeshawahi kufanya onyesho katika Mji huu wa Bukoba
kwani bendi hii ina historia nzuri katika muziki wa Tanzania haswa katika maonyesho yao mbalimbali ambayo wameshayafanya hapanchini.
Aidha Mc Jerry alisema kuwa ameamua kuwaletea wakazi hawa wa Mji wa Bukoba

bendi hii kwani bendi hii imekuwa inafanya vyema katika tasnia hii ya muziki wa dansi ambapo alifafanua kuwa kwa mwaka huu bendi hii ya Mashujaa inashikilia tuzo tano za muziki hapa nchini.
Alitaja kiingilio cha shindano hili ni shilingi10000 kwa kila mmoja huku akiwasihi wakazi wa mkoa wa Kagera kujitokeza kwa wingi kuangalia bendi hii ambayo inawanamuziki wengi ambao wanajua kutawala jukwaa kwa kuimba pamoja na kucheza.
5:51 AM
Unknown
Baada ya siku 11 ya matukio mbali mbali ya michezo 17 hatimaye sherehe za ufungaji wa mashindano zilifanyika katika uwanja wa Hampden Park siku ya Jumapili usiku huku wenyeji wa mashindano hayo Scotland wakimaliza wakiwa nafasi ya nne kwa kunyakua medali za dhahabu 19.
Huku England ikiwa nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza tangu miaka 28 iliyopita kwa kunyakua medali 58 za dhahabu, Australia ya pili kwa kuwa na medali 49 za dhahabu na Canada ikishika nafasi ya tatu kwa medali 32 za dhahabu.
5:51 AM
Unknown
Baada ya siku 11 ya matukio mbali mbali ya michezo 17 hatimaye sherehe za ufungaji wa mashindano zilifanyika katika uwanja wa Hampden Park siku ya Jumapili usiku huku wenyeji wa mashindano hayo Scotland wakimaliza wakiwa nafasi ya nne kwa kunyakua medali za dhahabu 19.
Huku England ikiwa nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza tangu miaka 28 iliyopita kwa kunyakua medali 58 za dhahabu, Australia ya pili kwa kuwa na medali 49 za dhahabu na Canada ikishika nafasi ya tatu kwa medali 32 za dhahabu.
5:47 AM
Unknown
Liverpool.

Dakika ya lala salama ya 88, Jesse Lingard anaongeza bao la tatu na kufanya 3-1 dhidi ya majogoo Liverpool. Bao hilo la Jesse lilihitisha ungwe hiyo ya pili United wakiibuka na ushindi na kujinyakulia kombe la kwanza chini ya uongozi mpya wa Kocha Lous Van Gaal.
Fainali hii ni ya kipekee sana!!!
Nyimbo za Mataifa yao ziliimbwa kabla ya mtanange kuanza...
Tayari mtanange kuanza...
Kikosi cha Liverpool
Steven Gerard akimfunga kipa wa United kwa mkwaju wa penati.Gerrard mapema aliwapachikia Liverpool bao kwa mkwaju wa penati na hapa alikuwa akipongezwa na Henderson na Lambert
Rooney akisawazisha bao na kufanya 1-1 baada ya kupata krosi safi kutoka kwa Hernandez's scross
Kutangulia siyo kufika: Rooney akiwawasha Liverpool
Mtajiju: Rooney akishangilia bao lake huko Miami baada ya kusawazisha
Juan Mata hakuchelewesha mambo ndani ya dakika 2 alitupia bao katika dakika ya 57 kipindi cha pili.

Mata akipongezwa na Wanaunited wenzake!
Gerrard akitupia
Wachezaji wa United wakijiuliza kwa nini!! baada ya kufungwa penati!!
Rooney
Kocha Van Gaal
Rooney chupucupu afunge bao hapa kwenye frii kiki
Hernandez mbele ya Skrtel
Shaw Ander Herrera akimwangaisha Jordan Henderson
Juan Mata tena na Martin Skrtel
Antonio Valencia
Ashley Young akichuana na Glen Johnson
Ashley Young na Glen Johnson
Luke Shaw wa Man United akiendesha..
VIKOSI:
MANCHESTER UNITED: De Gea, Evans (Blackett 46), Smalling, Jones, Valencia (Shaw 9), Herrera (Lingard 78), Fletcher (Cleverley 46), Young, Mata (Kagawa 68), Rooney [captain], Hernandez (Nani 68).
Subs: Lindegaard, Amos, Johnstone, M Keane, James, Zaha, W Keane.
Goals: Rooney (55), Mata (57), Lingard (88)
Booking: Shaw (52).
LIVERPOOL: Mignolet, Kelly, Johnson, Skrtel, Sakho (Toure 74), Gerrard [captain] (Lucas 62), Allen (Ibe 62), Henderson, Coutinho (Peterson 77), Lambert (Can 62), Sterling.
Subs: Jones, Coates, Coady, Phillips, Robinson, Suso.
Goal: Gerrard (14, pen)
Attendance: 51,104
MANCHESTER UNITED: De Gea, Evans (Blackett 46), Smalling, Jones, Valencia (Shaw 9), Herrera (Lingard 78), Fletcher (Cleverley 46), Young, Mata (Kagawa 68), Rooney [captain], Hernandez (Nani 68).
Subs: Lindegaard, Amos, Johnstone, M Keane, James, Zaha, W Keane.
Goals: Rooney (55), Mata (57), Lingard (88)
Booking: Shaw (52).
LIVERPOOL: Mignolet, Kelly, Johnson, Skrtel, Sakho (Toure 74), Gerrard [captain] (Lucas 62), Allen (Ibe 62), Henderson, Coutinho (Peterson 77), Lambert (Can 62), Sterling.
Subs: Jones, Coates, Coady, Phillips, Robinson, Suso.
Goal: Gerrard (14, pen)
Attendance: 51,104
4:42 AM
Unknown
Julio Grondora enzi za uhai wake
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia
salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio
Grondora.
Amesema
yeye binafsi na jamii ya mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla
wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa Rais wa Chama cha
Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).
Ameongeza
kuwa Grondora alikuwa mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani
alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu, na mchango wake katika
maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati wote.
Rais
Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata
pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya
FIFA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
cha msiba huo mzito.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.
4:40 AM
Unknown
Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo
BAADA ya Yanga sc kuenguliwa kushiriki michuano ya
klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati , maarufu kama Kombe la
Kagame, kwa kugoma kupelekea kikosi cha kwanza kama walivyoagizwa, Shirikisho
la soka Tanzania TFF, limesema klabu hiyo ina haki kutoshiriki mashindano kama
inaona haijajiandaa.
Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface
Wambura Mgoyo amezugumza na MPENJA BLOG
mchana huu na kueleza kuwa klabu inapokuwa bingwa, hakuna kanuni inayoibana
kwamba lazima ishiriki mashindo fulani, bali kama wanaona hawapo tayari
wanaweza kuwasiliana na TFF, halafu klabu nyingine inatafutwa.
“Tunachosema ni kwamba klabu inapokuwa bingwa sio
kwamba kuna kanuni zinailazimisha kucheza mashindano. Kwahiyo ikiona kwamba
haijajipanga kwa mashindano, bado ina haki ya kutuandikia sisi kuwa hawapo
tayari kushiriki mashindano na tunatafuta timu nyingine inayokwenda kwenye
mashindano,” alifafanua Wambura.
Hata hivyo, Shirikisho la soka Tanzania limeichagua
Azam fc kwenda kushiriki mashindano hayo na tayari limeshawaandikia barua baada
ya mawasiliano ya pande zote kwenda barabara.
“Ni kweli , CECAFA waliwapa Yanga muda wa
kuthibitisha kikosi chao, lakini muda umekwisha, maana yake sasa CECAFA
wamefanya uamuzi wa kuwatoa katika michuano ya Kagame kwa uamuzi wa kupeleka
kikosi cha pili au mchanganyiko kinyume na kanuni za mashindano. Na hii ililenga
kupunguza hadhi ya mashindano,” alisema Wambura.
“Kwahiyo CECAFA wakaiondoa Yanga na badala yake
sisi tukawaomba watupe hiyo nafasi kwa kutafuta timu nyingine ambayo
itatuwakilisha kwa maana ya Tanzania bara, tukasema lazima tuwe na uwakilishi
kwenye mashindano hayo na tumewapa nafasi Azam.”
“Tumeshawaandikia barua baada ya kuzungumza nao na
ndio watatuwakilisha kwenye mashindano yanayotarajia kuanza Agosti 8
“Cha msingi cha kuelewa ni kwamba kila mashindano
yana kanuni zake na taratibu zake. Kila mashindano lazima uwe na sifa ya
kushiriki, ukishakuwa na sifa, unatakiwa kufuata kanuni kama zinavyoelezeka”
Aidha, Wambura alisema TFF hawahusiki kwa lolote
kuhusu maamuzi hayo kwasababu wao sio sehemu ya waandaaji wa mashindano.
“Sisi kama TFF hatupo kwenye hayo mashindano na waliohusika kuwatoa Yanga ni waandaji wa mashindano, kwahiyo sisi hatuna lingine la kufanya isipokuwa kuwakumbusha watu kuwa wanapokwenda kucheza mashindano wazingatie kanuni na wasitunge kanuni zao, wanatakiwa kufuata kanuni za waandaaji”.
4:35 AM
Unknown
Wamekutana: Cristiano Ronaldo na James Rodriguez wakitoa dole kuashiria mambo 'supa' wakati wa mazoezi ya Real Madrid.
MWANASOKA BORA wa dunia, Cristiano Ronaldo amekutana na kijana mpya wa Real Madrid James Rodriguez katika mazoezi ya klabu hiyo mjini Madrid nchini Hispania.
Rodriguez alijiunga na mabingwa hao wa
Ulaya kutokea klabu ya Monaco kwa dau la paundi milioni 60 baada ya
kuonesha kiwango kikubwa katika fainali za kombe la dunia majira ya
kiangazi mwaka huu na kutwaa kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa
mashindano.
Baada ya mapumziko akitokea kombe la
dunia kuiwakilisha Colombia, nyota huyo aliripoti katika uwanja wa
mazoezi wa klabu hiyo wa Valdebebas HQ ambapo aliungana na wenzake.
Ronaldo akifanya mazoezi katika uwanja wa Valdebebas
Ona kitu hicho: Nyota wa Real (kutoka
kushoto) Ronaldo, Karim Benzema, Rodriguez na Raphael Varane wakati wa
mazoezi ya Real Madrid
Subscribe to:
Comments (Atom)
RSS Feed
Twitter