
5:13 AM

Unknown
JUMATANO
Klabu za Liverpool na Barcelona zilifanya mazungumzo kuhusu Uhamisho wa
Luis Suarez ambae kwa sasa yuko kwenye Kifungo cha Miezi Minne
alichopewa na FIFA kwa kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini
wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy huko Brazil.
Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Ian Ayre, alikutana na Maafisa kutoka Barcelona na mazungumzo zaidi yamepangwa.
Huku
pande zote zikitarajia kukamilika majadiliano yao haraka, inaaminika
Dau la kumuuza Suarez kutoka Liverpool kwenda Barcelona huenda likagonga
Pauni Milioni 70 kwani Liverpool wanataka Pauni Milioni 80 na Barca
wanadaiwa kukubali Pauni Milioni 60.
Chanzo
kutoka Anfield kilikaririwa kikisema: “Mazungumzo yalikuwa mazuri yenye
mafanikio na kila upande ulifikia matarajio yake. Mazungumzo zaidi
yatafanyika. Kwa sasa hakuna kilichokubaliwa.”
Inaaminika Barca wako
tayari kumtoa Winga wao kutoka Chile, Alexis Sanchez, kwa Liverpool
kwenye Dili ya kumchukua Suarez lakini pia mazungumzo hayo ya Jana
yaligusia kutoka Dau lote bila kuweka Mchezaji juu.
Lakini,
hata kama Barca watamnunua Suarez, Mchezaji huyo haruhusiwi kufanya nao
Mazoezi na hata kukanyaga Uwanjani kama Mtazamaji hadi baada ya Oktoba
26 atakapomaliza Kifungo chake cha Miezi Minne kilichoanza Juni 26.
Pamoja na Kifungo hicho, Suarez pia amefungiwa kucheza Mechi 9 za Nchi yake Uruguay na pia kutwangwa Faini Dola 111,000.
Baada
ya kukanusha kumuuma Chiellini, Juzi Suarez alimwomba radhi Mchezaji
huyo wa Italy pamoja na Ulimwengu wa Soka kitu ambacho kilikubaliwa na
Chiellini na Barca kukiita ni ‘unyenyekevu.’