Wednesday, May 27, 2015

Kocha wa Bournemouth ya England Eddie Howe Kocha wa timu ya soka Bournemouth ya England Eddie Howe ametajwa kuwa meneja bora wa mwaka wa shirikisho la mameneja wa soka nchini Uingereza LMA.Kutajwa kwa meneja huyo kunakuja kufuatia kuiongoza kwa mafanikio klabu yake ambayo imeingia ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza tokea ianzishwe zaidi ya miaka 100 iliyopita. Howe anakuwa kocha wa...
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika -CAF leo hii limeipa Tanzania uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019. Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali hizi. Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa...
Klabu ya Spain, Sevilla, Jumatano wanawania kuweka Historia ya kuwa Klabu ya kwanza kutwaa Kombe la EUROPA LIGI kwa mara ya 4 watakapokuwa ndani ya National Stadium Mjini Warsaw, Poland, kucheza Fainali na Klabu ya Ukraine, FC Dnipro Dnipropetrovsk. Sevilla wametwaa Kombe hili mara 3 katika Miaka ya 2006, 2007 na 2014. Mbali ya kuwania kuwa Klabu ya kwanza kulibeba Kombe mara 4, Sevilla...
Dutchman Mart Nooij, kocha wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, imeamua kuwa kocha Mkuu wa timu ya taifa Mart Nooij apewe changamoto ya kufaulu kucheza fainali za michuano ya CHAN mwakani, akishindwa aondoke. Nooij raia wa Uholanzi ambaye kikosi chake hakikufanya vizuri katika michuano ya kusaka taji la COSAFA...
Wachezaji wawili wa klabu ya soka ya TP Mazembe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiongozwa na mlinda mlango Robert Muteba Kidiaba, wamewasilisha maombi ya kuwania ubunge katika jimbo la Katanga. Pamoja na Kidiaba ambaye anafahamika sana kwa mtindo wa kusherehekea bao kwa kuruka kwa makalio, Pamphile Mihayo Kazembe pia ni mchezaji mwingine wa TP Mazembe anayewania ubunge kupitia...
Kocha wa Spain Vicente del Bosque amewaita Vijana wapya wawili wa Sevilla, Sergio Rico na Aleix Vidal, kwa ajili ya Mechi zao za Juni dhidi ya Costa Rica na Belarus na kumwacha Straika wa Chelsea Diego Costa.Kipa Rico, Miaka 21, na Winga Vidal, Miaka 25, wamekuwa waking'ara Msimu huu na Sevilla ambayo imemaliza La Liga ikiwa Nafasi ya 5 na Jumatano Mei 27 huko Stadion Narodowy Mjini...

waliotembelea blog