Friday, January 1, 2016


Baada ya dirisha dogo la usajili kwa Ligi Kuu soka Tanzania bara kufungwa December 15, barani Ulaya ndio stori za usajili zinazidi kuchukua nafasi. December 31 stori kutoka mtandao wa 101greatgoals.com unaripoti klabu ya Arsenal ya Uingereza imekamilisha mipango ya usajili ya Mohamed Elneny.
324742-fd3fdc1a3229a74b1eda5126005b0ca5
Dirisha dogo la usajili kwa nchi za Ulaya linafunguliwa January 1 klabu ya Arsenal inaripotiwa kukamilisha mpango wa kumsajili Mohamed Elneny kutoka klabu ya Basel ya Uswiss kwa kumfanyia vipimo vya afya leo December 31, hivyo Arsenal tayari imeshatenga dau la pound milioni 7.3 kukamilisha dili hilo.
2013_02_02_fcb_biel_0023
Arsene Wenger anatajwa kumsajili Mohamed Elneny staa wa Misri kutoka klabu ya Basel ili kuziba pengo la Santi Cazorla na Coquelin. Staa huyo wa Misri ambaye ana umri wa miaka 23, ameanza kuichezea timu ya taifa ya Misri toka mwaka 2011 na kucheza jumla ya mechi 39.



Mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico anayekipiga katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani Javier ‘Chicharito’ Hernandez, December 31 amerudi tena katika headlines za soka, baada ya mafanikio yake kuzidi kuonekana. Chicharito amerudi kwenye headlines baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi.
as
Kufuatia kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi, hii inatafsirika kama ishara aibu kwa kocha wa Man United Louis van Gaal ambaye alisababisha kuondoka kwa mchezaji huyo, kutokana na kauli yake ya kutompa nafasi ya kucheza na kumwambia kuwa hana nafasi katika kikosi chake.
Chicharito aliyeondoka Man United katika dirisha dogo la usajili la mwezi August 2015, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa wezi mara mbili mfululizo, baada ya mwezi November kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo.
Van-Gaal-Chicha
Kwa sasa Chicharito amecheza jumla ya mechi 14 akiwa na klabu ya Bayer Leverkusen  na kufanikiwa kushinda jumla ya goli 11, wakati mshambuliaji tegemeo wa Man United Wayne Rooney ameshinda goli 2 katika mechi 15 alizocheza. Hii inadhiirisha kuwa Van Gaal alifanya makosa kumuacha Chicharito aondoke.

waliotembelea blog