RAIS wa Shirikisho la Soka la Italy, FIGC, Carlo Tavecchio, amefungiwa Miezi 6 na UEFA kwa matamshi yake ya Kibaguzi.Tavecchio, mwenye Miaka 71, alitoa kauli ya Kibaguzi wakati wa Kampeni za Uchaguzi wake wa wadhifa huo Mwezi Julai alipotamka kuwa Wachezaji wa Kigeni ni ‘wala ndizi.’Baadae Mheshimiwa huyo aliomba radhi.Adhabu hii ya UEFA inamaanisha hawezi kushika wadhifa wowote wa UEFA...