Winga
anayechipukia wa Real Madrid, Jese Rodriguez ameweza kuziba pengo la
Cristiano Ronaldo vyema kipindi hiki ambacho anatumikia adhabu ya kadi
nyekundu. Kukosekana kwa Ronaldo kulitafsiriwa na wengi kuwa itakuwa ni
nafasi nzuri kwa Gareth Bale kuonekana, lakini Jesse ameweza kumfunika
vibaya Bale kiasi ambacho kimemfanya macho ya mashabiki kuhamia kwa
Jesse. Kutambua kiwango cha Jesse, kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti
pia ameanza kumpa kipaumbele mchezaji huyu kwa kumpa namba kwenye kila
mchezo. Jesse anaonekana kuwa ni mchezaji atakayeweza kusaidiana na
Ronaldo kuibeba timu na hakika nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya
taifa la Hispania itaonekana kwa kuanza kucheza kwenye kikosi cha
kwanza, kwani hadi sasa bado haiwahi kucheza kwenye timu ya kwanza ya
taifa.
Wednesday, February 19, 2014
9:36 PM
Unknown
Kikosi cha Arsenal kilichoanza
Kikosi cha Bayern Munich kilichoanza
Minong'ono
imeanza kuwa Robben alimtemea mate Sagna kama inavyoonekana kwenye
kiduara cha njano kwenye picha. Lakini baadhi ya watu wamesema ni jasho
lililokuwa linadondoka kutoka kwenye kidevu cha Robben.
Mkwaju huo umedakwa kwa kupanguliwa nje na kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer uliopigwa na Mesut Ozil katika dakika ya 8. Dakika ya 37 kipindi cha kwanza kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny anatolewa nje kwa kupewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia ndivyo sivyo Robben ndani ya eneo hatari, Mkwaju wa penati unatengwa. David Alaba anakosa penati mpira unagonga posti na kutoka nje!! Arsenal wanafanya mabadiliko Santi Cazorla anatoka na nafasi yake inachukuliwa na kipa Lukasz Fabianski katika dakika ya 39 kipindi cha kwanza na dakika ya 31 pia Arsenal walifanya mabadiliko ya Kieran Gibbs baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Monreal. Kosa kosa hizo za penati katika timu zote mbili zimesababisha timu zote kwenda mapumziko 0-0.
Mkwaju wa Ozil ukidakwa na kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer mapema kipindi cha kwanza!
Kipindi cha pili dakika ya 46 Bayern Munich wanafanya mabadiliko ya Jerome Boateng na nafasi yake
kuchukuliwa na Rafinha. Dakika ya 54 kipindi cha pili Toni Kroos akaifungia bao timu yake Bayern Munich baada ya kupewa pasi na Philipp Lahm.
Baadae kidogo Yaya Sanogo akapewa kadi ya njano baada ya kumchezea ndivyo sivyo kipa wa Bayern Munich Never. Dakika za
lala salama dakika ya 88 mchezaji wa Bayern Munich Thomas Müller aliyetokea benchi akaifungia bao timu yake, Bao la kichwa baada ya kupewa pasi safi na Philipp Lahm.
Kipa Szczesny akiruka na Arjen Robben...
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Wilshere, Oxlade Chamberlain, Ozil, Cazorla, Sanogo. Subs: Fabianski, Rosicky, Podolski, Giroud, Monreal, Jenkinson, Gnabry.
Bayern Munich: Neuer, Lahm, Boateng, Dante, Alaba, Thiago, Javi Martinez, Robben, Kroos, Gotze, Mandzukic. Subs: Starke, Van Buyten, Rafinha, Pizarro, Muller, Contento, Schweinsteiger.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Wilshere, Oxlade Chamberlain, Ozil, Cazorla, Sanogo. Subs: Fabianski, Rosicky, Podolski, Giroud, Monreal, Jenkinson, Gnabry.
Bayern Munich: Neuer, Lahm, Boateng, Dante, Alaba, Thiago, Javi Martinez, Robben, Kroos, Gotze, Mandzukic. Subs: Starke, Van Buyten, Rafinha, Pizarro, Muller, Contento, Schweinsteiger.
Mwamuzi:Nicola Rizzoli (Italy)
2:49 AM
Unknown
Kocha
wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson wiki hii ametembelea sehemu
tofauti nchini Brazil ambazo zitatumika na timu ya England kufanya
mazoezi, kucheza na kulala. Baadhi ya maeneo ambayo Roy ametembelea ni
pamoja na uwanja wa Arena Amazonia ambao England watafungua dimba dhidi
ya Italy na pia alitembelea miji ya Manaus, Rio de Janeiro, Sao Paulo na
Belo Horizonte. Katika mahojiano yake na waandishi wa habari baada ya
kuzungukia maeneo haya Roy alisema ' Brazil kuna joto sana, kama
ilivyokuwa South Afrika na America mwaka 94, lakini tulishacheza na
Brazil Rio de Janeiro naamini tutaweza kushindana kwenye hali hii'. Timu
ya England ipo kundi D pamoja na timu za Italy, Uruguay na Costa Rica.
Huu ni uwanja wa Arena Amazonia ambao England watafungua dimba dhidi ya Italy
Subscribe to:
Comments (Atom)
RSS Feed
Twitter




