Wednesday, July 1, 2015



Akimwaga wino kwenye karatasi kujiunga jumla na Klabu ya Liverpool kutokea Southampton

 Nathaniel Clyne akipozi kupata picha na Uzi wa Liverpool

Clyne amesaini mkataba wa miaka 5 kwa kitita cha  £12.5m

Clyne tayari amekamilisha mambo yake yote ikiwemo upimwaji na sasa yu Tayari kuleta mabadiliko kwenye Klabu mpya ya Liverpool.


Clyne ni miongo mwa wachezaji 6 waliosajiliwa na Liverpool kwa msimu wa 2015/2016


Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi za TFF zilizopo Karume, Tenga ameishukuru serikali ya Tanzania na TFF kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa, vyombo vya habari na wapenzi wa mpira wa miguu nchini kwa sapoti yao na kuipokea kwa mikono miwili michuano hiyo.
Lengo la CECAFA ni kuona vilabu vya ukanda huu vinapata nafasi ya kucheza michezo mingi na kujiandaa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru CECFA kwa kuipa Tanzania uenyeji huo na kuahidi TFF itahakikisha michuano hiyo inafanya nchini katika hali ya amani na usalama toka mwanzo mpaka mwisho wa michuano hiyo.
Timu zilizothibtisha kushiriki michuano hiyo ni Yanga, Azam (Tanzania), APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan), Al Shandy (Sudan) LLB AFC (Burundi), Heegan FC (Somalia), Malakia (Sudani Kusini), Adama City (Ethipia) na KCCA (Uganda).
Wakati huo Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ametangza ratiba ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es salaam ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa CECAFA.


Wachezaji wa Argentina wakipongezana baada ya kuifunga bao 6-1 ParaguayNdani ya Estadio Municipal Alcaldesa Ester Roa Mjini Rebolledo Nchini Chile, Argentina wameitandika  Paraguay katika Nusu Fainali ya Pili ya Copa America. BAO za  Argentina  zimefungwa na
Marcos Rojo 15'
Javier Pastore 27'
Ángel Di María 47' 
Ángel Di María 53 

Bao la Paraguay limefungwa na Lucas Barrios dakika ya 43 kipindi cha kwanza.
Ushindi wa Argentina asubuhi hii kuifanya kwenda nusu Fainali na kukutana uso kwa uso na Wenyeji Chile ambao wametinga Fainali baada ya kuichapa Peru 2-1.Lionel Messi
Baada ya kukutana awali katika Mashindano haya na kutoka Sare 2-2 katika Mechi ya Kundi lao ambayo Argentina waliongoza Bao 2-0 kabla Haftaimu na Paraguay kusawazisha, safari hii pia Argentina waliongoza 2-0 kwa Bao za Marcos Rojo na Pastore, zilizotengenezwa na Nahodha wao Lionel Messi.


tr
Dwayne  Johnson maarufu kama The Rock ni mwigizaji, producer wa movie na mchezaji wa mieleka kutoka Marekani aliyejitengenezea jina kubwa kwenye mieleka na baadae tukaanza kumwona kwenye movie za action HollywoodMarekani.
The Rock alichukua time na kufanya interview na gazeti la Esquire la Marekani na kuongelea mambo mengi ikiwemo sababu zilizomfanya aingie kwenye movie na kusahau kabisa ishu za mieleka.
ex
Dwayne Johnson kwenye movie ya The Expendables 3.. Pembeni yake yuko Bruce Wills.
Baada ya kufanikiwa kwenye mieleka, nilihamasika kujaribu kucheza movie za action, na nimefika hapa nilipo kutokana na nidhamu niliyojifunza kwenye mieleka, kujenga ukaribu na watu kwenye industry, na kujiunga na madarasa ya kuigiza>>> Hapa amenukuliwa The Rock kwenye moja ya Interview zake.
gi
The Rock kwenye action
Anapendelea nini kati ya mieleka na action movies? >>> “Mieleka ni mpenzi wangu wa kwanza, lakini kwenye action kuna upendo tofauti ambao unaniruhusu mimi kugusa watu kupitia sanaa nyingine na pia kutengeneza hela ndefu zaidi, movie zinanifundisha mambo mengi sana ambayo nisingeweza kuyajua mwanzoni“.
saaaaan
Hapa ni kwenye movie aliyoigiza 2015 SAN ANDREAS, moja ya movies ziliofanya vizuri Marekani.

waliotembelea blog