Mchezo huu ukiongozwa na Mwamuzi Jonas Eriksson
Tuesday, November 17, 2015
10:26 PM
Unknown
MAGOLI:
Goli la kwanza limefungwa dakika ya 1 na Yacine Brahimi
la pili likifungwa dakika ya 23 na Faouzi Ghoulam, Bao la tatu dakika ya 43 limefungwa na Riyad Mahrezna hivyo kwenda mapumziko Tanzania ikiwa nyuma ya bao 3-0 nyuma ya Wenyeji wao Algeria. Bao la (4)nne limefungwa na Slimani islam kwa mkwaju wa penati dakika ya 49 na kufanya Algeria kuongoza bao 4-0.
Faouzi Ghoulam alifunga tena bao kwa mkwaju wa penati dakika ya 59. Dakika ya 72 bao tena kupitia kwa Carl Medjani. Dakika ya 75 Slimani islam anaifungia bao la 7 na kufanya 7-0(Agg 9-2).
KADI ZA NJANO:
Farid Mussa, Himid Mao, Kelvin Patrick Yondani, Haji Mngwali, Mudathiri Yahya na dakika ya 41 tena Mudathiri Yahya alifanya rafu tena na kuoneshwa kadi ya njano ya pili na kutolewa na mwamuzi Neant Alioum kwa kadi nyekundu.
Kipindi cha pili dakika ya 48 Nadir Haroub alioneshwa kadi ya njano. Dakika ya 57 Aishi Manula nae analambishwa njano.
RED KADI:
Mudathiri Yahya Dakika ya 41
10:25 PM
Unknown
Mchezaji wa timu ya mpira wa Kikapu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ephraim Mlawa (kushoto) akichuana na Juvenary Shichose wakati Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo hicho lililofanyika, mwishoni mwa wiki katika Kituo cha Michezo cha JMK Youth Park na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kutoa vifaa vya michezo kwa timu zilizoshiriki mchezo wa soka. (Picha na Francis Dande)
Timu za mpira wa kikapu kutoka Chuo cha IFM zikichuana katika Bonanza la michezo la wanafunzi wa chuo hicho.
Kikosi cha timu ya Soka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), BBF kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha timu ya Soka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), DIT kikiwa katika picha ya pamoja.
Mshauri wa wanafunzi wa Chuo cha IFM, Khamis Kihongoa akikagua timu ya DIT wakati wa Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo cha IFM.
Mshauri wa wanafunzi wa Chuo cha IFM, Khamis Kihongoa akikagua timu ya DIT wakati wa Bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo cha IFM.
Mshambuliaji wa timu ya DIT, Shaban Juma (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya BBF, Yohana Galus wakati wa bonanza la michezo la wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
10:23 PM
Unknown
Kwa mujibu wa Takwimu za CIES Football Observatory Digital Atlas, Asilimia 41 ya Wachezaji waliocheza Ligi Kuu England Msimu huu wamechezea pia Timu zao za Taifa Msimu huu huu.
Man United wapo juu kwa kutoa Wachezaji Asilimia 72 ya wale walioteuliwa na Meneja wao Louis van Gaal kucheza Mechi za Ligi Kuu England Msimu huu ambao pia waliteuliwa kucheza Timu zao za Taifa.
Ijumaa
iliyopita, Wachezaji wa Man United waliovaa Jezi za Nchi zao ni Michael
Carrick, Phil Jones, Chris Smalling, Wayne Rooney na Juan Mata ambao
walicheza wakati Spain inaichapa England 2-0, wakati Anthony Martial na
Morgan Schneiderlin walikuwa kwenye France iliyoichapa Germany ambayo
ilikuwa nayo Bastian Schweinsteiger huku Daley Blind akiichezea
Netherlands na Matteo Darmian akiichezea Nchi yake Italy.
10:21 PM
Unknown
Stars inayonolewa na kocha mzalendo, Charles Boniface Mkwasa iliwasili salama jana jioni katika mji wa Blida, uliopo takribani kilometa 75 kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Houari Boumediene jijini Algiers.
Mkwasa amesema mchezo huu watajituma kadri ya uwezo kuhakikisha wanapata ushindi, makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa awali yamefanyiwa kazi na anaamini vijana wake watapambana kusaka ushindi katika mchezo huo.
Wachezaji wote 21 wapo katika hali nzuri, hakuna mchezaj majeruhi hata mmoja, hivyo kocha Mkwasa ana wigo mpana wa kumtumia mchezaji yoyote anayemuhitaji kwa ajili ya mchezo huo.
Mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018, utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Mali na utaanza saa 1:15 usiku (Algeria) sawa na saa 3:15 usiku kwa saa nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki.
10:21 PM
Unknown
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah Kibadeni ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kujiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza kutimua vumbi Jumamosi Novemba 21, nchini Ethiopia.
Kibadeni anayesaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, amesema wachezaji aliowaita wapo katika hali nzuri na wamekua wakifanya mazoezi na kikosi cha Taifa Stars ambapo wao kama benchi la ufundi wamepata nafasi ya kuwa nao kwa muda mrefu na kutambua maendeleo yao.
“Tumechagua wachezaji kulingana na mahitaji ya timu, tumekua na wachezaji hawa kwa muda mrefu katika vipindi mbalimbali, tuna amini tuliowachagua watafanya vizuri katika michuano hiyo mikongwe barani Afrika” amesema Kibadeni.
Wachezaji walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa), Juma Abdul (Yanga) na Kelvin Yondani (Yanga).
Viungo Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba), Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Deus Kaseke (Yanga), washambuliaji John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga) na Saimon Msuva (Yanga).
Michuano ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 na kumalizika Disemba 6, ambapo Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A, lenye wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.
Wachezaji Said Mohamed, Juma Abdul, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Salum Abubakar na Ibrahim wanaendelea na mazoezi jijini Dar es salaam chini ya kocha msaidizi Juma Mgunda wakati wanawasubiri wachezaji wengine walioko nchini Algeria na kikosi cha Taifa Stars.
Kundi B lina Bingwa Mtetezi Kenya, Burundi, Uganda na Zanzibar, huku kundi C likiundwa na timu za Sudan, Sudani Kusini, Djibouti na waalikwa wa michuano hiyo timu ya taifa kutoka Malawi.
10:20 PM
Unknown
Katika michezo iliyochezwa jana matokeo yalikuwa ni Alliance 2 -0 Madini, JKT Rwamkoma 1- 3 Bulyanhulu, Mvuvuma 0 – 0 Green Warriors, Singida United 1 -0 Transit Camp, Mirambo 1 – 0 Abajalo Tabora.
Karikaoo 1 – 0 Cosmopolitan, Mshikamano 1- 1 Changanyikeni, Villa Squad 0 – 2 Abajalo Dar es salaam, Mkamba Ranger 0 -0 The Mighty Elephant, Sabasaba 0 - 1 Mbeya Warriors, Wenda 0 – 0 African Wanderes.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea Novemba 28, kwa timu 24 kucheza katika viwanja 12 mbalimbali nchini kusaka pointi muhimu.
10:12 PM
Unknown
Mfalme mzee Yusuphy akiwa anawatumbuiza wapenzi wa bendi ya Jahazi modern taaraba Woinde
Shizza,Arusha
Bendi ya
muziki wa taarabu ijulikanayo kwa jina la Jahazi modern taarab inayomilikiwa na mfalme mzee yusuphy inatarajia kutua rasmi
jijini Arusha kwa ajili ya kuitambulisha album mpya inajulikana kwa jina la Mahaba
niuee.
Akizungumza
na waandishi wa habari muandaaji wa onyesho hilo ambaye ni mkurugenzi wa phide
entertainment, Phidesia Mwakitalima alisema kuwa bendi hiii ya jahazi inatarajiwa kutua jijini
Arusha na kufanya onyesho lao December 11
ambapo litafanyika ndani ya ukumbi wa Triple A com lex uliopo ndani ya
jiji hili.
Alisema kuwa
mpaka sasa utaratibu wote umekamilika na wanangoja tu siku ya onyesho ambapo
alieleza kuwa onyesho hili litakuwa rasmi kwa ajili ya kutambulisha albamu mpya
ya jahazi pamoja na kutambulisha nyimbo zilizopo katika alibamu hiyo.
Aidha
alitaja baadhi ya nyimbo zilizopo katika albamu hiyo na ambazo zitatambulishwa
kwa wapenzi wa jahazi modern taarabu kuwa ni pamoja na nyimbo iliyobeba albamu Mahaba niueee,alibainisha kuwa pamoja na
uzinduzi huu hii pia itakuwa ni sehemu
ya ziara yao kufunga mwaka Tanzania nzima kwa bendi hii ya muziki wa Taarabu.
Phidesia
aliwasihi wakazi wa mji wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wajitokeze kwa
wingi kwani wasanii wote ,waimbaji wote wacheza show wote na wake wote wa mzee
yusuphy watakuwepo katika onyesho hilo.
Aliwataja
baadhi
ya wadhamini wa onyesho hilo kuwa ni pamoja na Geo security, kwa
udhamini mkubwa wa Geo Security Arusha kampuni
bora ya ulinzi, security power fance na alarm ambapo alisema na katika
siku hiyo ya onyesho watakuwepo pia kwa ajili ya usalama wa wapenzi
wote kuhakikisha mnarudi salama majumbani salama .
Subscribe to:
Comments (Atom)
RSS Feed
Twitter