Thursday, December 19, 2013



LISTI YA FIFA YA UBORA DUNIANI iliyotolewa leo bado ina Mabingwa wa Dunia, Spain, kama ndio Nambari Wani na wapo hapo kwa Mwaka wa Sita mfululizo.
Tanzania imepanda Nafasi 4 na sasa ipo Nafasi ya 120 huku Ivory Coast bado ikiendelea kukamata Nafasi ya 17 ikiwa ndio Timu ya Juu kabisa toka Barani Afrika.

Listi nyingine ya Ubora itatolewa Tarehe 16 Januari 2014.
20 BORA:
1  - Spain
2  - Germany
3  - Argentina
4  - Colombia
5  - Portugal
6  - Uruguay
7  - Italy
8  - Switzerland
9   - Netherlands
10  - Brazil
11   - Belgium
12  - Greece
13  - England
14  - USA
15   - Chile
16  - Croatia
17  - Côte d'Ivoire
18  - Ukraine
19  - Bosnia and Herzegovina
20  - France
TANZANIA ILIPO:
116    Malawi
116    Latvia
118    Mozambique
119    Sudan
120    Tanzania
121    New Caledonia
121    Lebanon


KIUNGO mahiri wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere amekubali adhabu aliyopewa na Chama cha Soka cha Uingereza-FA lakini atapinga adhabu ya kufungiwa mechi mbili aliyopewa. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza alikuwa akituhumiwa kuonyesha ishara ya matusi kwa mashabiki wa Manchester City katika uwanja wa Etihad baada ya timu yake kupewa kipigo cha mabao 6-3 katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika wiki iliyopita. Tukio hilo halikuonwa na mwamuzi wa mchezo huo lakini picha za video zilimuonyesha Wilshere akitoa ishara hiyo na FA kumpatia adhabu kwa sheria mpya ambayo huwaruhusu kufanya hivyo kama tukio halikuonekana na mwamuzi. Kesi yake inatarajiwa kusikilizwa Alhamisi na kama adhabu ikibaki hivyo nyota huyo anatarajiwa kukosa mechi mbili za Ligi Kuu ukiwem mchezo dhidi ya Chelsea Desemba 23 na mchezo dhidi ya West Ham United siku tatu baadae.Jack Wilshere alivua jezi baada ya kibano cha bao 6-3 kutoka kwa City.


Pichani kulia ni aliyewahi kuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006,Jokate Mwegelo akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali mapema leo Mikocheni jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa klabu yake iliyojulikana kwa jina la KIDOTI CLUB,Shoto ni mmoja waratibu,Mtangazaji wa East Africa Radio aitwaye Bhoke.

Mmoja wa Mashuhuda akitoa ushuhuda wake mara baada ya kujiunga kwenye klabu ya KIDOTI CLUB,kwa njia ya simu kwa kutuma neno KIDOTI kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.

Baadhi ya wanahabari waliofika kwenye uzinduzi huo uliofanyika Mikocheni,jijini Dar.
Baada ya kutamba na mitindo ya nywele na nguo aina ya Kidoti brand, msichana mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha klabu yake ijulikanayo kwa jina la Kidoti Club.

Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo jana, Jokate alisema kuwa Kidoti Club ni tofauti na vilabu vingine kwani katika ujio wake huo mpya, atakuwa anajihusisha na mambo mbali mbali katika jamii hususani masuala ya urembo na mitindo. Jokate pia alizindua aina mpya ya nywele zake za kisasa katika mtindo wa kidoti Brand.

Jokate alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri mbali mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwa ajili ya rika tofauti. Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na anaamini watu wengi watajiunga naye.

Kwa mujibu wa Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, ili uwe mwanachama wa klabu hiyo, unatakiwa kutuma neno kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.

“Huu ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii,Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake, mimi pia naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu mbali mbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi. Alisema kuwa pia ataendesha mashindano mbali mbali kwa wanachama wake na kutoa zawadi kwa washindi.

“Kama unavyojua, lengo langu kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji chake kwa watanzania wote, nataka wafaidike na vipaji vyangu name kusimama mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu yoyote, natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa wabunifu katika kukabiliana na masuala mbali mbali ya maisha,” alisema.

Saida Karoli 

MSANII wa muziki wa asili aliyewahi kutamba na wimbo wa ‘Maria Salome’ uliokuwa maarufu kwa jina la ‘Chambua Kama Karanga’, Saida Karoli amesema umaarufu aliokuwa nao haukufanana na kile alichokitia mfukoni.
Mkali huyo wa Kaisiki na Mapenzi kizunguzungu alisema alitembea nchi nyingi duniani bila kuingiza kipato kikubwa mfukoni mwake kutokana na kulipwa mshahara na meneja wake hata kama angefanya kazi kubwa na shoo zilizoingiza kipato kikubwa.
“Siwezi kuweka wazi mshahara niliolipwa ila nakumbuka nilifanya shoo za kulipwa kwa dola na kuzunguka nchi mbalimbali duniani ila nililipwa kwa fedha ya Kitanzania tena mshahara uleule kila mwezi, nashukuru kwa sasa ninajisimamia mwenyewe ninapata fedha nyingi sana ingawa sina jina kama zamani,” aliweka wazi Saida Karoli.
Kwa sasa msanii huyu ameweka makazi yake jijini Mwanza huku akitamba na wimbo wa Mashamsham na albamu yake ya Pesa Inawasha.


Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Desemba 21 mwaka huu) ni sh. 5,000. Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 40,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja katika vituo mbalimbali, mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Vituo ambavyo tiketi hizo zitauzwa keshokutwa (Ijumaa) ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.

Mechi hiyo itachezeshwa na Ramadhan Ibada (Kibo) kutoka Zanzibar, ambapo atasaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba, na Simon Charles kutoka Dodoma. Mwamuzi wa akiba ni Israel Nkongo wa Dar es Salaam wakati mtathimini wa waamuzi ni Soud Abdi wa Arusha.
 

waliotembelea blog