
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini
ya miaka 17 (Serengeti Boyz) inacheza mechi ya kujipima nguvu kesho
(Julai 11 mwaka huu) dhidi ya Azam U-20 kwenye Uwanja wa Azam Complex,
Dar es Salaam. Mechi hiyo ambayo ni maalumu kwa benchi la ufundi la
Serengeti Boyz likiongozwa na kocha Hababuu Ali Omari kuangalia kikosi
chao itaanza saa 2 kamili asubuhi. Serengeti Boyz itacheza mechi...