Friday, July 3, 2015

Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Akizungumza katika Uzinduzi Huo Akiwa na   Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula (Kushoto) Pamoja na Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole.
Simba Sports Club kwa kushirikiana na Kampuni ya Tigo Tanzania zimezindua huduma ya ujumbe mfupi ijulikanayo kama ‘SIMBA NEWS’, ambayo lengo lake nikuwapatia wateja wa Tigo taarifa zinazoihusu klabu ya Simba popote walipo nchini.
Huduma hii mpya inajulikana kama ‘SIMBA NEWS’. Njia hii ni rahisi na yenye ufanisi yenye kuifanya dunia ijulikane kwa wateja wake. “Pamoja na kasi yaukuaji wa Tehama, Tigo inaelewa umuhimu wakutoa taarifa kwa wateja wake, ndiyo maana leo, tunajisikia fahari kuzindua huduma hii iliyotengenezwa vizuri ya SIMBA NEWS nawashirika wetu wa klabu ya SIMBA, EAG Group LTD pamoja na Premier Mobile Solutions (PMS), ilikuendelea kuwapa wateja wetu taarifa zinazohusu masuala ya sasa huku wakifurahia habari mpya zinazohusu klabu,”alisema meneja wa mawasiliano ya kibiashara Jacqueline Nnunduma.
Lengo letu si tu kuwapatia wateja wetu taarifa kiurahisi zaidi, lakini pia kuwapatia taarifa hizo kwa wakati na zenye uhakika kutoka vyanzo vya michezo vyenye kuaminika,” aliongeza Nnunduma.
Akizungumza kwa niaba ya Klabu ya Simba,Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva alisema, “Tunaamini ubunifu huu bila shaka utawawezesha mashabiki wote wa Simba na wa soka kwa ujumla ambao pia ni wateja wa Tigo kupata habari mbalimbali za klabu ya Simba kupitia simu zao za mkononi”.
Tunawahimiza mashabiki wetu kujiunga na huduma hii kupitia Tigo ili waweze kupata nakufurahia habari mbalimbali kutoka klabu ya Simba. Aliendelea Aveva.
Akiongea katika tukio hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa shughuli za kibiashara na masoko katika klabu ya Simba, alisema “Tunatarajia kuendelea kuwapatia mashabiki wa Simba huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia zisizokuwa na usumbufu wa aina yeyote kupitia wadau wanaoaminika ndani ya Tanzania”
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole alisema kuwa huduma hii imetengenezwa ili kuwawezesha wateja kupata habari za papo kwa papo naaliongeza kuwa huduma ipo katika mfumo wa vifurushi vya Combo / BUNDLE PACK ambapo wateja wa Tigo watakuwa wakilipia mara moja kwa siku na kupokea kiwango cha chini cha habari nne (04) na habari mpya za kila siku zina zohusu klabu ya Simba.
Huduma pia itamruhusu mteja aliyejiunga kujitoa kwenye huduma hii wakati wowote akitaka bila vikwazo vyovyote na pia kwenye huduma hii kutakuwepo na neon kuu “MSAADA”kwa ajili ya kusaidia juu ya maswali mbalimbali ya nayo ulizwa mara kwa mara na wateja wakati wakifurahia huduma.
Ili kujiunga na huduma hizi unatakiwa kutuma neon kuu SIMBA kwenda 15460. Utakapo jiunga tu mteja atapokea habari kutokana na neon analolituma kila siku na atatozwa kiasi cha shilingi za kitanzania 150 kwa siku. Na ili kujitoa kwenye huduma mteja atahitaji kutuma neno ONDOA SIMBA kwenda 15,460.


Mchezaji wa klabu ya Manchester United Nani anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa matibabu katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahce baada ya vilabu hivyo viwili kukubaliana ada ya yuro milioni 6 kwa uhamisho wa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alihamia Manchester United kutoka klabu ya Sporting Lisbo ya Ureno.
Alicheza msimu uliopita katika kilabu ya Sporting Lisbon na kufanikiwa kufunga mabao 11.
Fenerbahce inasema kuwa mazungumzo ya uhamisho wa mchezaji huyo yanaendelea na kwamba Nani atakuwa mjini Istanbul ili kufanyiwa ukaguzi wa matibabu.
Nani ameshinda mataji manne ya Ligi ya Uingereza na moja la vilabu bingwa Ulaya akiichezea Manchester United.
Alitia sahihi mkataba wa miaka mitano na kilabu hiyo mwaka 2013



Paul Pogba
Mgombea wa wadhfa wa urais katika klabu ya Barcelona Joan Laporta anasema kuwa mabingwa hao wa Ulaya watajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Juventus Paul Pogba iwapo atachaguliwa.
Ripoti zinasema kuwa kilabu ya Barcelona ilijaribu kumsajili raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 ambaye aliisaidia Juventus kushinda ligi ya Serie A na kufika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.
''Kuna mchezaji tunayempenda sana -Paul Pogba. Tunamjua ajenti wa mchezaji huyo na hilo na swala muhimu katika oparesheni zetu. Tutajadiliana na wakala wake pamoja na klabu ya Juventus'',. Alisema Laporta.

Siku ya Jumatano, Vyombo vya habari Nchini Uhispania na Italy vilisema kuwa Barcelona imetoa kitita cha yuro milioni 80 kwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United ambaye pia anahusishwa na uhamisho katika vilabu vya Chelsea na Manchester City.


Aliyekuwa mchezaji wa vilabu vya Arsenal na Chelsea Nicolas Anelka amechaguliwa kama mkufunzi wa klabu ya Mumbai City.
Anelka mwenye umri wa miaka 36 aliichezea klabu hiyo ya ligi kuu nchini India chini ya ukufunzi wa aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Manchester City Peter Reid.
''Alituvutia sisi sote na ufundi wake pamoja na ujuzi wa hali ya juu alionao'',alisema mmiliki wa kilabu hiyo ambaye pia ni mwigizaji nyota wa Bollywood Ranbir Kapoor.
Anelka alikuwa mchezaji mkufunzi katika kilabu ya Shanhai Shenhua mwaka 2012.

Raia huyo wa Ufaransa alifanikiwa kufunga mabao mawili pekee katika mechi saba alizocheza katika msimu wake wa kwanza mjini Mumbai lakini anarudi katika kilabu hiyo kama mchezaji ambaye anafaa kulipwa mshahara mkubwa.

Anelka was unveiled as Mumbai City's new manager via their official Twitter feed with a cartoon depiction of the Frenchman wearing a smart, black suit

Na Saleh Ally
ULIMSIKIA yule mchezaji kinda wa Yanga, Geofrey Mwashiuya aliyesema kwamba hata Yanga anapita, yuko njiani kwenda Ulaya ambako amekuwa na ndoto ya kucheza soka la kulipwa?


Mwashiuya ambaye amejiunga na Yanga msimu huu akitokea timu ya daraja la kwanza ya Kimondo, aliyasema hayo mbele ya waandishi wa habari kwamba Yanga anapita!

Kinda huyo ambaye ameonyesha kuwa ana kipaji hadi kuzua gumzo, aliwaambia Kimondo kwamba wamuache acheze Yanga badala ya kuendelea kulumbana, lakini akawa mstaarabu na kutoa shukurani kwao kwa kumlea katika kipindi cha misimu miwili alichoichezea timu hiyo.

Baada ya hapo, ndiyo akatoa kauli hiyo kwamba Yanga anapita. Yeye ndoto yake imekuwa ni kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Kweli wachezaji wengi Watanzania wamekuwa na ndoto za kucheza soka la kulipwa barani Ulaya lakini kuzungumza tu imekuwa shida na hiyo ni sehemu ya kuonyesha kwamba hawajiamini.

Wengi wamekuwa wakizungumzia ndoto zao baada ya kustaafu. Utasikia: “Nilikuwa na ndoto ya kucheza Ulaya lakini hata hivyo mambo hayakwenda vizuri. Wakati wetu pia ilikuwa shida sana!”

Unawajua wachezaji wangapi ambao wanaona kuchezea Yanga au Simba ndiyo mwisho wa safari? Wanaona kufikia kuchezea timu hizo, basi hakuna sababu tena ya kuendelea kutafuta kwingine.

Kweli Yanga na Simba ndiyo klabu kongwe na zenye mashabiki wengi zaidi lakini hakuna ubishi ni lazima kwa mchezaji yeyote bora kuvuka mipaka ili kutafuta mafanikio zaidi.

Kwangu alichokisema Mwashiuya kinaonyesha namna alivyo na moyo mpana, namna alivyo na pumzi ya kutosha kwenye ubongo wake na anavyoweza kufikiria mambo mengi na kutaka kuyafanyia kazi.

Huenda anaweza kuwa mchezaji wa kwanza au wa mwisho kusema Yanga anapita akiwa hata hajapata uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza.

Wengine wote wangezungumzia namna wanavyoweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza na kuitumikia Yanga kwa nguvu zote ikiwezekana kuisaidia kuipa ubingwa.

Kauli ya “Yanga napita”, ina mengi ambayo yamejumlishwa zaidi na yale ambayo yangeweza kusemwa na wengine kwani inaonyesha ili apite Yanga, lazima afanikiwe. Ili afanikiwe lazima ajitume, apate namba ya uhakika, aisaidie Yanga kufanya vizuri halafu aonekane.

Kwangu namuona ni kijana jasiri sana. Nilisoma makala ya Edibily Lunyamila katika Gazeti la Championi la juzi akimueleza kinda huyo mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutolewa sifa mapema ambazo zimewaangusha wengi sana.

Sioni sababu ya kuyarudia yote ambayo Lunyamila alimueleza Mwashiuya, lakini ukweli yalikuwa ni sehemu ya maneno bora ambayo anaweza kuyachukua na yakasaidia kumjenga na kumfanya awe imara katika safari yake ya kuiwinda Ulaya.

Kikubwa ni kumpa ushirikiano, kama kipaji chake kinafanya kazi basi aungwe mkono kwa kuwa akishatoka nje ya Tanzania, hatakuwa wa Yanga tena, badala yake atakuwa ni mchezaji kutoka Tanzania na kwa faida ya taifa letu ambalo linahitaji wachezaji wengi waende nje ya Tanzania.

Kikubwa ambacho ninaweza kumkumbusha ni kwamba safari hiyo ya kwenda Ulaya haiwezi kuwa rahisi au laini kama ambavyo anafikiria. Kuna milima na mabonde na haitakuwa rahisi kwa kuwa si kila mmoja hata wengine walio Yanga watafurahia yeye kuona anakwenda Ulaya.

Dunia ina watu tofauti sana, wenye husda, wenye roho mbaya na wasiopenda maendeleo ya wengine. Mara zote huwa wanazidiwa nguvu na ukweli na hasa kama yeye atafanya kazi yake akiwa ana malengo kweli ya kuvuka na kufika anapotaka kwenda.

Kumuomba Mungu ni jambo muhimu katika kila kitu, lakini Mwashiuya lazima akubali kwamba utulivu wa akili, kujituma na nidhamu ya hali ya juu ni baadhi ya mambo muhimu yatakayomfikisha katika ndoto yake ya kupita Yanga na kwenda kucheza Ulaya.



Mshambuliaji Hamisi Kiiza amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba ya Dar es Salaam.

Kiiza amesaini mkataba huo baada ya kufuzu zoezi la vipimo jijini Dar es Salaam.

Kiiza ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Yanga aliwasili jana akitokea nchini Uganda kwa ajili ya vipimo na kumalizia mazungumzo na uongozi wa Simba.

Akiwa nchini, Kiiza alisema amekuja kufanya kazi na Simba.


Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Tido Mhando amesema wataboresha matangazo ya Ligi Kuu
KITUO cha Televisheni cha Azam kimepania kuboresha matangazo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia msimu ujao, kuhakikisha yanaptikana katika ubora wa hali ya juu.
Kwa ujumla, Azam TV inayofukuzia miaka miwili tangu ianzishwe imejipanga kuwapatia Watanzania matangazo ya ubora wa kiwango cha juu sana wakati wote wa kipindi cha msimu huu wa mchakato wa uchaguzi mkuu wabunge na Urais mwaka huu wa 2015.
Mtendaji Mkuu Uhai Productions, wazalishaji wa vipindi vya Azam TV, Dunstan Tido Mhando amesema leo kwamba kwa kuwa tukio hili ni la kihistoria, Azam TV pia imedhamiria kutoa matangazo ya kihistoria kwa ubora na ufanisi ukilinganisha na aina ya matangazo ya televisheni ya matukio kama haya katika miaka ya nyuma.
Kwa kutumia teknolojia ya kisasa, vifaa bora pamoja na wafanyakazi wenye ujuzi na weledi, Azam TV hasa kwa kutumia channel yake ya Azam TWO, itatangaza matangazo ya uchaguzi wa mwaka huu kwa kipindi chote cha Uchaguzi kwa kuanzia na harakati za hivi sasa za kutangaza nia kwa wagombea mbalimbali hasa wale wa nafasi ya Urais kutoka chama tawala cha CCM na baadaye kambi ya Upinzani.
Azam Televisheni imejipanga kutangaza mfulilizo wa Matangazo ya Moja kwa moja kutoka Dodoma kwa kutumia vipindi vyake mbalimbali pamoja na vipindi vingine maalum, pilikapilika zote, harakati zote pamoja na matokeo yote ya kilele cha mpambano huo wa hatimae kupatikana kwa mgombea huyo wa Urais wa CCM.
Kuanzia Jumatano July 8 hadi Jumatatu July 13 kikosi cha wafanyikazi wa Azam Televisheni kitapiga kambi Dodoma kueleza kwa kinaga ubaga kila jambo litalokuwa linatokea huko na kwa undani sana ikitumia wachambuzi wenye ujuzi pamoja na kupata na kuzitoa habari za uhakika kwa haraka iwezekanavyo.
Matangazo haya yataanzia tangu mapema asubuhi kwenye kipindi chake cha matangazo ya asubuhi kijulikanacho kama Morning Trumpet, kipindi maalum cha saa moja wakati wa mchana kuanzia saa saba, kipindi cha jioni cha Alasiri Lounge, taarifa ya habari maalum ya saa mbili kutoka saa
mbili kamili usiku pamoja na kipindi maalum cha usiku kuanzia saa nne na nusu hadi saa sita usiku.
Wakati wa kilele cha hekeheka hizi za huko Dodoma yaani tarehe 11 July na 12 July ambapo mkutano mkuu wa CCM unafanyika, Azam Televisheni itakuwa na matangazo ya moja kwa wakati wote wa mkutano huo na baadae.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huu, Azam Televisheni itatangaza pia mikutano na mipango mingine kama hii kwa upande wa vyama vingine vya kisiasa.
Utaratibu wa matangazo haya ya uchaguzi utaendelea hivi hivi wakati wa kipindi chote cha kampeni kuanzia mwezi wa August hadi tarehe yenyewe ya uchaguzi hapo Octoba 25.
Labda ni wakati wa kipindi hicho cha uchaguzi kamili ambapo Azam televisheni imejiimarisha zaidi kuweza kuwapatia watazamaji wake matangazo bora ya kisasa zaidi kuliko wakati wowote katika historia ya utangazaji nchini hapa.
Kwa kuzingatia umuhimu wa uchaguzi na upatikanaji wa habari za uhakika kwa watanzania Azam imeweka dhamira hii kama sehemu ya historia kwa kutimiza wajibu wa msingi wa vyombo vya habari kwa umma wa watanzania.
Kwa kutumia studio bora kuliko zote karika kanda hii ya Afrika pamoja na vifaa vingine vya kileo kabisa, Azam televisheni itatangaza mfulilizo na moja kwa moja matukio yote muhimu ya wakati huo wa kupiga kura, kuhesabiwa kwa kura na hatimae kutangazwa washindi wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar, Wabunge wa bunge la Muungano na Baraza la wawakilishi, Zanzibar.
Kujiamini huku kwa Azam Televisheni katika kutekeleza lengo hili kubwa kunafuatia kuajiriwa kwa kundi la watangazaji mahiri ambao kwayo ujuzi na uelewa wao pamoja na misingi ya weledi itakayozingatiwa bila ya shaka utawezesha ari hii kutekelezwa kwa kiwango cha mafanikio makubwa.
Miongoni mwa watangazaji hao ni Charles Hilary, Ivona Kamuntu, Fatuma Nyangassa, Baruani Muhuza, Hassan Mhelela, Faraja John, Raymond Nyamwihula, Jane Shirima, Phillip Cyprian, Mwanga Kirahi, na Taji Liundi.
Tuna amini ya kwamba kundi la watangazaji hawa wenye ujuzi na wengine wachache ambao watakuja hivi karibuni wakiungana na wale vijana wasomi ambao tayari wamekuwepo wataweza kufanikisha ile ari ya kukifanya kituo cha Azam Televisheni kuwa bora zaidi katika kanda hii.
Mbali na kuimarishwa kwa kitengo cha habari lakini mipangp na mikakati bora imeandaliwa ya kupata vipindi vingine bora vya aina mbalimbali ambavyo vitatayarishwa kwa kiwango cha juu na cha hadhi ya kimataifa ikiwa ni pamoja na kuimarishwa kwa kiasi kikubwa kwa matangazo ya vipindi vya michezo na matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ikiwa ni pamoja na yale ya ya ligi kuu ya kandanda Tanzania yaani Vodacom Premier League.
Kwa kuwapatia watazamaji wetu na watanzania kwa ujumla matangazo haya bora ya vipindi vizuri vya televisheni, tunauhakika wanunuzi wa ving’amuzi vya Azam watakuwa wanapata wakitakacho na zaidi.

KLABU ya Chelsea imemsajili Radamel Falcao kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Monaco, huku kinda wa Blues, Mario Pasalic akihamia kwa wapinzani kama sehemu ya makubaliano ya dili hilo.
Mshambuliaji huyo wa Colombia atacheza Ligi Kuu ya England kwa msimu wa pili akiwa na kikosi cha Jose Mourinho, baada ya kushindwa kung'ara akiwa na Manchester United msimu uliopita.
"Nina furaha sana kujiunga na Chelsea na nina hamu ya kuanza mazoezi na kusaidia dhamira yetu ya kutetea ubingwa na kupata mafaniko Ulaya," amesema Falcao.
Chelsea goalkeeper Thibaut Courtois saves from Falcao last season; the two will now be reunited in London
Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois akiokoa dhidi ya Radamel Falcao msimu uliopita; wawili hao sasa wanaungana London

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, aliitua Old Trafford msimu uliopita kama mmoja wa washambuliaji tishio Ulaya, lakini maumivu ya goti aliyoyapata wakati anacheza Monaco yalionekana kumpunguza makali.
Kinda Mcroatia, Pasalic, ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Elche katika La Liga, sasa atakwenda kwa mkopo Monaco kama sehemu ya dili hilo.
Falcao ataungana na Diego Costa, Thibaut Courtois na Filipe Luis, ambao wote wamewahi kuchezea Atletico Madrid, sambamba na mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Colombia, Juan Cuadrado Uwanja wa Stamford Bridge. 


CHAMA cha Soka Ivory Coast kimetoa orodha fupi ya walimu watano wanaowania nafasi ya kuwa Kocha Mkuu wa Tembo, iliyoachwa wazi na mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Mfaransa Herve Renard.
Imeelezwa kigezo kinachotumika kumpata kocha mpya wa Tembo ni uzoefu wa kufanya kazi Afrika na uwezo wa kuzungumza Kifaransa kwa ufasaha ili iwe rahisi kwake kuwasiliana siyo tu na wachezaji wa Ulaya, bali hata wa nyumbani.
Henryk Kasperczak  ambaye aliifundisha Ivory Coast kati ya mwaka 1993 na 1994, anakamilisha idadi ya makocha watano walioingia fainali. 
Mpoland huyo mwenye umri wa miaka 68 pia amewahi kufanya kazi timu za taifa za Tunisia, Mali na Senegal.
Kocha wa zamani wa Guinea, DRC na Mauritania, Patrice Neveu, sambamba na Michel Dussuyer, aliyeiongoza Guinea katika AFCON ya mwaka 2015, yumo katika tano bora.
Kocha Mreno, Paulo Duarte, aliyewahi kufundisha Burkina Faso na Gabon, pia anawania kuwa kocha wa Ivory Coast, wakati kocha wa zamani wa klaba za Rennes na Nice za Ufaransa, Frederic Antonetti ndiye pekee kati ya wanafainali, ambaye hajawahi kufanya kazi Africa.
FA ya Ivory Coast ilipokea jumla ya maombi ya makocha 60, lakini imewapunguza hadi kubaki watano wiki hii.
Mabingwa hao wa Afrika kwa sasa hawana kocha Mkuu kuelekea mchezo wa pili kufuzu AFCON mwishoni mwa mwaka.
RAIS wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni atahudhuria mchezo wan chi yake dhidi ya Tanzania, Taifa Stars kesho Saa 10:00 jioni Uwanja wa Nakivubo, Kampala.
Mecho hiyo ya kesho ni mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2016 Rwanda na mgeni rasmi atakua Rais Museveni.
Kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Boniface Mkwasa, kiliwasili jijini Kampala jana usiku na kimefikia katika hoteli ya Grand Global iliyopo jirani na chuo kikuu cha Uganda Makerere.
Taifa Stars imefanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Nakivubo yakiwa ni mazoezi mepesi na mwisho kuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe utakaofanyika kesho jioni.
Rais Museveni (kushoto) akipiga danadana mbele ya wachezaji wa The Cranes miaka miwili iliyopita. Kesho atakuwapo uwanjani vijana wake wakimenyana na Taifa Stars
Wachezaji wa Taifa Stars wakifanya mazoezi leo mjini Kampala

Kocha Mkwasa akiongelea kuelekea mchezo huo amesema, anashukuru vijana wake wamefika salama wote, hali nzao ni nzuri, morali ni ya hali ya juu, kikubwa wanatambua wana deni kubwa kwa watanzania hivyo kesho watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Akiongelea hali ya hewa na mazingira ya timu ilipofikia, Mkwasa amesema hali ya hewa ni ya kawaida baridi na mvua kidogo haina tofauti sana na Tanzania, mazingira ya hoteli ni mazuri na kusema kikubwa kilichobaki ni kusaka ushindi katika mchezo huo na vijana wake wapo tayari. 
Wakati huo huo mashabiki zaidi ya 50 kutoka nchini Tanzania wanatarajiwa kuwasili kesho jumamosi alfajiri wakitokea jijini Dar es salaam kuungana na watanzania wengine waishio nchini Uganda kuishangilia timu ya Tanzania itakapokuwa ikipimbana na Uganda katika uwanja wa Nakivubo.
Taifa Stars inatakiwa kushinda maba4-0 ili kusonga mbele, baada ya awali kufungwa mabao 3-0 Zanzibar wiki mbili zilizopita. Baada ya kipigo hicho, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimfukuza kocha Mholanzi, Mart Nooij na wasaidizi wake wote na kumteua Mkwasa, ambaye anasaidiwa na Hemed Morocco, kocha wa makipa Manyika Peter chini ya Mshauri wa Ufundi, Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden'. 



Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi za TFF zilizopo Karume, Tenga ameishukuru serikali ya Tanzania na TFF kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa, vyombo vya habari na wapenzi wa mpira wa miguu nchini kwa sapoti yao na kuipokea kwa mikono miwili michuano hiyo.

Lengo la CECAFA ni kuona vilabu vya ukanda huu vinapata nafasi ya kucheza michezo mingi na kujiandaa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru CECFA kwa kuipa Tanzania uenyeji huo na kuahidi TFF itahakikisha michuano hiyo inafanya nchini katika hali ya amani na usalama toka mwanzo mpaka mwisho wa michuano hiyo.

Timu zilizothibtisha kushiriki michuano hiyo ni Yanga, Azam (Tanzania), APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan), Al Shandy (Sudan) LLB AFC (Burundi), Heegan FC (Somalia), Malakia (Sudani Kusini), Adama City (Ethipia) na KCCA (Uganda).

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ametangaza ratiba ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es salaam ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa CECAFA.

Mechi ya ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam itashuhudia wenyeji Yanga SC wakicheza na Gor Mahia ya Kenya, huku APR ya Rwanda ikicheza na Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua dimba na Telecom ya Somalia.

Ratiba ya michuano hiyo imeziweka timu hizo katika makundi matatu ambapo kundi A lina timu za: Yanga (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djbiout), KMKM (Zanzibar) na Khartoum-N (Sudan)

Kundi B: APR (Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB AFC (Burundi) na Heegan FC (Somalia), Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda)

Timu tatu zitakazoshika nafasi ya juu kutoka kundi A, timu mbili za juu kutoka kundi B & C, na mshindi mwenye wastani mzuri kutoka kundi B & C zitaingia katika hatua ya robo fainali.

BENDERA AIPONGEZA TFF
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dokta, Joel Bendera ameipongezs TFF kwa kuandaa mashindano ya ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13),  na maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika za vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

 Bendera amesema hiyo ndiyo njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio pia amepongeza juhudi za Chama cha Soka mkoa wa Manyara na TFF kwa kuandaa kozi za makocha na waamuzi, akisema huo ndiyo uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya soka mkoani Manyara.

Aidha aliwaasa makocha kutumia mbinu za kisasa za ufundishaji soka walizozipata kwenda kuendeleza vipaji vya wachezaji watakaowafundisha.

Pia Bendera amewahakikishia wakazi wa Manyara atahakikisha wanaandaa vipaji vitakvyowawezesha kuwa na timu bora itakayowakilisha mkoa wa Manyara.

ACCREDITATION FOR ALL AFRICAN GAMES:
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limetangza kufunguliwa kwa maombi ya vitambulilsho kwa wandishi wa habari kwenye fainali za michezo ya Afrika zitakazofanyika mwezi Septemba mwaka huu nchini Congo- Brazaville.

Waandishi wa habari wanaotajiwa kwenda kufanya kazi kwenye michuano hiyo wanaombwa kufanya maombi ya vitambulisho (Accrediatation) kuanzia Juni 29 mpaka Julai 7 mwaka huu


TAIFA2
Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager kesho jumamosi saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimba la Nakivubo kucheza na wenyeji Uganda.(The Cranes).
Mecho hiyo ya kesho ni mchez wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2016 zitakazofanyika mapema mwezi Januari nchini Rwanda, mgeni rasmi atakua Rais wa Uganda Yoweri Mseveni.
Kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa, kiliwasili jijini Kampala jana usiku na kimefikia katika hoteli ya Grand Global iliyopo jirani na chuo kikuu cha Uganda Makerere.
TAIFA2
Taifa Stars imefanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Nakivubo yakiwa ni mazoezi mepesi na mwisho kuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe utakaofnayika kesho jioni.
Kocha Mkwasa akiongelea kuelekea mchezo huo amesema, anashukuru vijana wake wamefika salama wote, hali nzao ni nzuri, morali ni ya hali ya juu, kikubwa wanatambua wana deni kubwa kwa watanzania hivyo kesho watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Akiongelea hali ya hewa na mazingira ya timu ilipofikia, Mkwasa amesema hali ya hewa ni ya kawaida baridi na mvua kidogo haina tofauti sana na Tanzania, mazingira ya hoteli ni mazuri na kusema kikubwa kilichobaki ni kusaka ushindi katika mchezo huo na vijana wake wapo tayari. 
Wakati huo huo mashabiki zaidi ya 50 kutoka nchini Tanzania wanatarajiwa kuwasili kesho jumamosi alfajiri wakitokea jijini Dar es salaam kuungana na watanzania wengine waishio nchini Uganda kuishangilia timu ya Tanzania itakapokuwa ikipimbana na Uganda katika uwanja wa Nakivubo.


Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Adv. Anthon Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpira wa Miguu kuwania Kombe la DC na kushirikisha timu 24 kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo jana.
Timu za Mpwapwa Academy na Kota FC zikizubiri kukaguliwa na mgeni rasmi. Katika mchezo huo wa ufunguzi Kota FC wqalishinda goli 3-2.
DC akikaribishwa kusalimiana na wachezaji.
Mdhamini wa michuano hiyo ya DC Cup 2015, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Anthony Mavunde akisalimia wachezaji wa Kota FC.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Anthony Mavunde akisalimia wachezaji Mpwapwa FC
Wachezaji wa Mpwapwa FC wakiwa tayari kuanza pambano lao.
DC Mavunde akipata maelezo kutoka kwa viongozi wa mpira Mpwapwa.

IMG-20150703-WA0036
Mara nyingi tunasikia stori kuhusu watu kukamatwa na dawa za kulevya kwenye viwanja vya ndege, wapo wanaotoka TZ kwenda nje na wapo wanaokamatwa wanaziingiza pia kutoka nje ya nchi.. nina hii stori kutoka ITV kuhusu mtu kukutwa na bangi ndani ya basi.
IMG-20150703-WA0037
Basi la Maning’inice lilitoka Mtwara kwenda Dar, njiani kulikuwa na Checkpoint ya Polisi ambapo jamaa aliyebeba bangi kwenye begi aliomba akajisaidie, Polisi walipoingia kwenye gari kukagua wakakutana na begi hilo lililojaa bangi na jamaa mwenye nalo alikuwa ameshakimbia tayari.
IMG-20150703-WA0038
Kuna mtu mmoja aliteremka akasema ana mkojo.. Askari akauliza nani mwenye hili begi yule jamaa akaanza kukimbia vichakani. Askari wakakimbizana nae maporini, akatokomea“– amesimulia dereva wa basi hilo, Hashim Mohamed.
IMG-20150703-WA0030
IMG-20150703-WA0029
Bangi iliyokutwa kwenye begi hilo ina uzito wa kama kilo 25 hivi… Stori hiyo nimeirekodi kwenye Habari iliyoruka ITV, na haoa utaisikiliza yote kwenye hii sauti.


1435763437-1799191-10153367464034788-3843205048929530093-o
Wapo wanaoogopa kusafiri kwa ndege kabisa, lakini haimaanishi kwamba usafiri wa ndege ni hatari au sio salama kabisa, kwa wataalam wanasema ndege ndio usafiri salama namba moja Duniani.
Ripoti za 2015 zimetoka, Qatar Airways imetajwa kama Shirika la Usafiri wa anga ambao ni bora zaidi duniani, najua wako ambao hawajawahi kusafiri kwa ndege za Qatar.
Kama unatamani kuyaona mazuri mengine yaliyomo ndani ya ndege hizo unaweza kuona pichaz zake hapa jinsi kulivyo humo ndani.
a-clever-little-storage-area-holds-amenity-kits
Pembeni ya siti kuna hii sehemu ambayo unaweza kuweka vitu vyako vidogo vidogo, vinakuwa salama kabisa safari yote
business-class-isnt-so-shabby-either
economy-class-is-also-excellent
Economy Class, sehemu ya kawaida na bado unaenjoy. Kila siti na TV yake.
economy-seats-feature-extra-cushy-headrests
every-seat-in-economy-has-a-power-outlet-usb-plug-and-even-a-personal-phone-that-lets-you-send-and-receive-text-messages-during-your-flight (1)
first-class-seats-can-be-flattened-into-actual-beds-so-its-easy-to-sleep-and-pajamas-and-slippers-are-complimentary
Kwenye utakavyoenjoy First Class ni pamoja na hii sehemu ambayo unaweza kulala kabisa ukiwa kwenye safari ndefu.
if-youre-thinking-these-look-like-bucket-seats-youre-not-wrong-qatar-claims-to-have-been-inspired-by-the-automotive-industry-when-designing-the-seats
Kwenye siti yako, wewe na TV yako kwa amani kabisa.
in-business-and-first-class-passengers-get-fresh-flowers-chandeliers-sumptuous-leather-seats-top-shelf-liquor-and-canaps
Ni kama hauko kwenye ndege yani.. Hapa vinywaji vyote vipo humohumo ndani ya ndege.
some-business-class-seats-are-extra-wide-and-feature-a-180-degree-lie-flat-bed
the-first-class-cabin-on-the-a380-is-pretty-swanky-the-seats-are-ultrawide-and-there-are-dividers-between-them-so-that-you-can-shut-out-chatty-neighbors-or-conversely-you-can-extend-the-table-to-hav
the-first-class-lounge-has-leather-benches-that-are-a-welcome-break-on-long-flights
watching-a-movie-on-a-plane-will-never-be-like-a-trip-to-the-cinema-but-these-screens-are-pretty-massive
Hapa sio kama Cinema eti wote muangalie movie moja, kila TV na movie yake.
Utaogopa kula chakula kwenye ndege ya Kichina? Ona mtu wangu, vyakula vya ndani ya Qatar vya kawaida kabisa, hata wali upo!!
the-kit-kat-is-a-nice-touch
255 imepiga stori na 255 Mb Dog amesema bado ana mpango wa kuendelea kufanya kazi na msanii mwenzake Madee kwa sababu ni mtu wake wa karibu ingawa hawajakaa karibu kwa muda mrefu.
Pia Stori za mitaani zinazungumza kuwa Video ya ‘Nana’ ya Diamond kacopy Video ya ‘Moyo wangu’..mwenyewe amesema wakati anatoa wimbo wa Moyo wangu hakuwa anajulikana sana kimataifa kama sasaivi na alichokifanya kwenye wimbo wake mpya wa Nana kaamua kuiboresha na kuiongezea ubunifu kwa kuchua vitu vichache kwenye wimbo wa Moyo wangu.


 


Stori nyingine ni kumhusu msanii Bele 9 ambaye kwa sasa ameamua kukaa kimya kujihusisha na mitandao ya kijamii na kusema hatumii kabisa..ameamua tu kurefresh na kufanya vitu vingine.. sasa anatarajia kutoa wimbo mpya na anaamini hawezi kuwa busy na mitandao alafu akafanya kitu kizuri kwa umakini
Kasema huwezi kuwa busy na mitandao ya kijamii alafu ukafanya kitu kwa umakini.






Straika wa Mexico Javier Hernández 'Chicharito' amevunjika mfupa wa begani na kufanyiwa operesheni ambayo itamweka nje kwa Wiki 4 na kukosa kuichezea Nchi yake Mashindano ya CONCACAF Gold Cup.
Chicharito aliumia Jumatano iliyopita huko Houston, USA wakati wa Mechi ya Kirafiki na Honduras iliyoisha 0-0 na kutolewa nje Dakika 5 kabla Haftaimu.
Msimu uliopita, Chicharito, mwenye Miaka 27 na ambae ni Fowadi wa Manchester United, alikuwa na Real Madrid kwa Mkopo na alipaswa kurudi Old Trafford huku kukiwa na fununu za mipango ya kumuuza.

Lakini kuumia kwake na kufanyiwa operesheni iliyomwekea chuma kwenye mfupa wa begani kutamweka nje kwa Wiki 4 na hali hii itafanya mipango hiyo ya Uhamisho wake isitishwe.Kukosekana kwa Chicharito pia ni pigo kwa Mexico kwani ni Mfungaji wa Bao 40 katika Mechi 73 za Nchi hiyo na walimtegemea sana kwenye Mashindano ya CONCACAF Gold Cup ambalo ni Kombe la Mataifa ya Nchi za Marekani ya Kaskazini, ya Kati na Visiwa vya Carribean yakatayochezwa Julai 7 hadi 26 huko Canada na United States.Mexico wako Kundi C na wataanza kwa kucheza na Cuba hapo Julai 9 huko Chicago kisha kuzivaa Guatemala na Trinidad and Tobago.
Kocha wa Mexico Miguel Herrera amemwita Javier Orozco wa Klabu Bingwa ya Mexico Santos Laguna kumbadili Chicharito.

waliotembelea blog