Friday, July 3, 2015



CHAMA cha Soka Ivory Coast kimetoa orodha fupi ya walimu watano wanaowania nafasi ya kuwa Kocha Mkuu wa Tembo, iliyoachwa wazi na mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Mfaransa Herve Renard.
Imeelezwa kigezo kinachotumika kumpata kocha mpya wa Tembo ni uzoefu wa kufanya kazi Afrika na uwezo wa kuzungumza Kifaransa kwa ufasaha ili iwe rahisi kwake kuwasiliana siyo tu na wachezaji wa Ulaya, bali hata wa nyumbani.
Henryk Kasperczak  ambaye aliifundisha Ivory Coast kati ya mwaka 1993 na 1994, anakamilisha idadi ya makocha watano walioingia fainali. 
Mpoland huyo mwenye umri wa miaka 68 pia amewahi kufanya kazi timu za taifa za Tunisia, Mali na Senegal.
Kocha wa zamani wa Guinea, DRC na Mauritania, Patrice Neveu, sambamba na Michel Dussuyer, aliyeiongoza Guinea katika AFCON ya mwaka 2015, yumo katika tano bora.
Kocha Mreno, Paulo Duarte, aliyewahi kufundisha Burkina Faso na Gabon, pia anawania kuwa kocha wa Ivory Coast, wakati kocha wa zamani wa klaba za Rennes na Nice za Ufaransa, Frederic Antonetti ndiye pekee kati ya wanafainali, ambaye hajawahi kufanya kazi Africa.
FA ya Ivory Coast ilipokea jumla ya maombi ya makocha 60, lakini imewapunguza hadi kubaki watano wiki hii.
Mabingwa hao wa Afrika kwa sasa hawana kocha Mkuu kuelekea mchezo wa pili kufuzu AFCON mwishoni mwa mwaka.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog