Tuesday, August 25, 2015

Klabu ya Juventus ya Italia bado inaongeza nguvu katika kikosi chake kwa kusajili wachezaji kadhaa ili kuweza kuendana na kasi ya michuano mbalimbali itakayoshiriki msimu huu. Juventus ambayo imeondokewa na nyota kadhaa kikosini mwake ikiwemo Carlos Tevez na Andre Pirlo imeongeza nguvu katika kikosi chake. Juventus August 25 wamekamilisha usajili wa mkopo kwa...
Mshambuliaji Pape Abdoulaye N'Daw mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kutua leo usiku kutoka Dinamo Bucuresti ya Romania kufanya majaribio Simba SC  SIMBA SC imeachana na Msenegali, Papa Niang baada ya kumjaribu kwa dakika 45 tu jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hawajachoka, Simba SC leo wanatarajia kupokea wachezaji...
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM ALIYEKUWA kipa wa Simba SC kwa misimu mmoja nusu uliopita, Ivo Philip Mapunda (pichani kushoto) amesema anarejea Kenya, baada ya kuachwa na klabu hiyo mapema mwezi huu. Ivo aliyewahi kudakia pia Yanga SC, amesema hana kinyongo na Simba SC na anaondoka nafsi yake ikiwa safi kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine. “Nawashukuru mashabiki wa mpira haswa wa Simba...
Diamond Platnumz ameamua kumtambulisha msanii wake wa kwanza mtu wangu kutoka kwenye lebo yake ya WCB,msanii huyu anaitwa Harmonize na hii ni singo yake ya kwanza inaitwa Aiyola,ukiisikiliza unaweza kuandika comment hapo chini. ...
Klabu ya soka ya Simba mwishoni mwa wiki iliyopita ilimleta mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Papa Niang ambaye ni ndugu wa damu na Mamadou Niang mchezji aliyetamba katika vilabu kadhaa barani Ulaya ikiwemo timu ya taifa ya Senegal. August 24 Papa Niang alijaribiwa na wekundu hao wa msimbazi katika mechi ya kirafiki ya Simba dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga...
Mgombea Urais wa UKAWA 2015 Edward Lowassa alianza ziara ya kuingia mitaani Dar es salaam Aug 24 2015 ili kukutana na Wananchi uso kwa uso na kusikiliza matatizo yao.  Lowassa amesema atatusaidia, tuna furaha sana leo ametutembelea, hatukutarajia,” alisema mwanafunzi wa Shule ya Nyegulu, Dorcus Wilson baada ya kuzungumza na Lowassa. Mwanafunzi mwingine wa Shule ya Msingi Maarifa, Grey Issa...
Mshambuliaji mtukutu ambaye amewahi kuvichezea vilabu kadhaa Mario Balotelli ameondoka Liverpool na kurejea katika klabu yake ya zamani ya AC Milan, Balotelli anarudi AC Milan ikiwa ni msimu mmoja umepita toka ajiunge na Liverpool akitokea AC Milan ya Italia kwa dau la pound milioni 16. akiwasili kwa kufanya vipimo vya afya Milan Balotelli anarudi Italia katika klabu ya AC Milan kwa...
NAHODHA wa zamani wa Arsenal, Mfaransa Thierry Henry anaamini klabu hiyo inapaswa kutumia kipindi kilichobaki kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba 2 kununua kiungo na mshambuliaji. The Gunners ililazimishwa sare ya bilakufungana na Liverpool usiku wa jana, licha ya kutawala sana mchezo kipindi cha pili, huku kipa Petr Cech akiokoa michomo miwili ya hatari mno ya Christian...
Omar Wayne (aliyeruka juu) amepelekwa kwa mkopo Majimaji ya Songea MAJIMAJI ya Songea mkoani Ruvuma imesajili wachezaji wawili wa Azam FC kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu- beki Ismail Gambo ‘Kussi’ na kiungo Omary Wayne. Wawili hao matunda ya akademi ya mabingwa hao wa Afrika Mashariki na kati tayari wamesafiri kwenda Songea kujiunga na Majimaji iliyorejea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania...
KIPA anayeonekana kuwa bora zaidi kwa sasa, Aishi Manula (pichani kushoto) wa Azam FC ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichopo kambini Uturuki.  Taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, imesema kwamba Aishi Manula hakuweza kusafiri na timu kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia katika mchezo...
Manchester United wameripotiwa kutoa Ofa inayokaribia Pauni Milioni 140 kumnunua Straika wa Barcelona ambae ni Kepteni wa Brazil, Neymar, kwa mujibu wa Chombo cha Habari cha huko Brazil Globo Esporte. Inaaminika Mkataba wa Barcelona na Neymar, mwenye Miaka 23, una kipengele kinachotaka Mabingwa hao wa Spain walipwe Dau la Pauni Milioni 140 ikiwa atataka kuhama kabla Mkataba kumalizika. ...
FULL TIME: ARSENAL 0 vs 0 LIVERPOOL, HAKUNA MBABE EMIRATES! Kipa Petr Cech ndie aliyeilinda Arsenal usiku huu kutofungwa Alexis Sanchez akijituma Wakati Liverpool hawajapoteza hata Mechi moja kwenye Ligi Msimu huu baada ya kushinda Mechi 2 na hii Sare na sasa wako Nafasi ya 3 wakifungana na Man United, Arsenal wao wako Nafasi ya 9 wakiwa wamefungwa Mechi 1, Ushindi 1 na Sare 1. Arsenal...
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro tayari imewasili salama nchini Uturuki katika mji wa Kartepe - Kocael leo mchana, tayari kwa kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017. Msafara wa Taifa Stars uliopoa nchini Uturuki unaongozwa na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF, Ahmed Mgoyi...

waliotembelea blog