Habari
zimetujia sasa hivi zinasema abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu
na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya
ndege waliyokuwa wakisafiria kuwa pasuka matairi yote manne ya nyuma
wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Arusha leo mchana.
Ndege
hiyo ya shirika la ndege la precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo
wakati ikitua, ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka na
kusababisha taharuki kubwa kwa abiria.
"Yaani
Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi
chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama
mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.
Mh
Lowassa ni mbunge wa Monduli, jimbo ambalo anatoka Waziri Mkuu
aliyekuwa kipenzi Cha mwalimu Nyerere na watanzania hayati Edward
Moringe Sokione.Sokoine aliyefariki katika ajali ya gari mwaka 1994.
UPDATES KUTOKA ABIRIA MWINGINE:Nikiwa
mmoja wa abiria tuliosafiri na PW kurudi Arusha leo, ndege ya shirika
hilo yenye usajili No 5HPWI imepata kizaazaa wakati wa kutua baada ya
tairi mojawapo kupasuka kwa kishindo, likufuatiwa na mengine yote ya
nyuma ambapo yalipasuka pia na kuacha vipandevipande kwenye njia ya
kurukia.
Waliookota
vipande hivyo wamesema kuwa wamekuta viraka(pechi, watu wa magari
wananielewa zaidi hapa), kitu ambacho si kawaida kwenye usafiri wa jamii
hii!
Rubani
wa ndege hiyo amejitahidi kuitoa ndege hiyo nje ya njia ili kutozuia
ndege nyingine kuruka, japokuwa mwishowe ilimgomea kabisa na kubaki
ikisota pembeni mwa njia hiyo.
Kikubwa ni kwamba hakuna madhara yaliyowapata abiria, akiwemo Bwana Lowassa.