
Jeneza lenye mwili wa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM,Marehemu Kapteni John Komba likiwa
kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam,wakati wa shughuli ya
kuaga.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za
mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la
Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya
Nyasa Mkoani Ruvuma.
Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na wake zake Mama Asha na
Mama Zakhia wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John
Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es Salaam leo.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassa Mwinyi akitoa heshima za
mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la
Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna
Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John
Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa
wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John
Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es Salaam leo.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,Luteni
Kanali Samuel Ndomba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu
Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh.
Jenista Mhagama akitoa heshima za mwisho akifuatana na Naibu
IGP,Abdulrahman Kaniki.
Kingunge Ngombale–Mwiru akitoa heshima za mwisho.
Kamanda Kova.
Baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wakiifariji familia ya Marehemu.
Mhe. Ole Sendeka akibubujikwa na machozi kuondokewa na Mbunge mwenzake.