
MSHAMBULIAJI
wa timu ya Stand United,Abasarim Chidiebele akizungumza na waandishi wa
habari mkoani Tanga mara baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa
kuitumikia timu ya Coastal Union,Picha na Mwandishi Wetu,Tanga

MSHAMBULIAJI
wa timu ya Stand United, Abasarim Chidiebele, amesaini mkataba wa
kuitumikia timu ya Coastal Union kwa mkataba wa mwaka mmoja katika msimu
ujao wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Chidiebele alitua mkoani
Tanga juzi kwa ajili ya kuingia makubaliana na uongozi wa timu ya
Coastal Union ambapo utiliaji saini huo ulishuhudiwa na viongozi
mbalimbali akiwemo Katibu wa Coastal Union, Kassim El Siagi, Meneja wa
Coastal Union, Akida Machai na viongozi wengine.
Akizungumza mara
baada ya kusaini, Chidiebele amesema kuwa amefurahi kusajiliwa na
Coastal Union na kuhaidi kutumia uwezo wake aliokuwa nao kwa ajili ya
kuipa mafanikio timu hiyo katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao.