
MCHEZAJI mstaafu wa timu ya soka ya KMKM Ali Issa Simai, amefariki dunia
jana wakati wa magharibi baada ya kuugua kwa muda mfupi, na kuzikwa leo
huko Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja.
Marehemu, ambaye alijulikana zaidi kwa jina la ‘Kepteni’ kutokana na
kuwa nahodha wa KMKM kwa muda mrefu, alikutwa na mauti nyumbani kwake
Fuoni baada ya kurudi kutoka katika shughuli zake za kawaida....