Sunday, January 10, 2016


 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari  mapema leo,alipokutana nao na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabiri tasnia hiyo,mkutano huo umefanyika kwenye moja ya ukumbi ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari 
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano ulioitishwa na Waziri Nape kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kati ni Waziri Mh.Nape pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akitoa muongozo kwa Wahariri wa Vyombo vya habari (hawapo nchini) kuhusina na mkutano wao ulioitishwa na Waziri Nape kujadili mambo mbalimbali na changamoto zinazoikabiri tasnia hiyo kwa ujumla.
 Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano uliohusu kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda na kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa .
 Mmoja wa Wahariri Kurwa Kaledia kutoka New Habari Hause akiomba ufafanuzi wa jambo kwa Mh Waziri Nape huku baadhi ya wahariri wakifuatilia kwa makini.
 Mmoja wa Wahariri Grace Hoka akifafanua jambo kwenye mkutano huo
 Baadhi ya Wahariri wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
 Baadhi ya Wahariri juu pichani wakishiriki kuchangia mambo mbalimbali kwenye mkutano huo.
 Mmoja wa Wahariri akifafanua jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya Wadau wakubwa wa habari pia walikuwepo kwenye mkutano huo

Msafara wa magari uliokuwa umembeba Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Wachezaji wa Ndani 2015, Mbwana Samata,ulionaswa na Camera ya Globu ya jamii maeneo ya Morocco jana jioni ukitokea hoteli ya Kempinsk baada ya kuzungumza na vyombo vya habari,Msafara huo akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye ulipita maeneo kadhaa ya jiji la Dar na kukomea katika kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar,ambako alikutana na kupongezwa na Wadau mbalimbali wa tasnia ya Michezo.Mwanasoka huyo aliwasili juzi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam akitokea Abuja, Nigeria katika hafla ya utoaji tuzo kwa mwanamichezo bora.
PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
Baadhi ya Waendesha Boda boda nao hawakuwa na hiyana kuunga mkono mafanikio ya Mbwana Samatta,ambayo yameiletea heshima kubwa nchi yetu.
Msafara wa Mbwana Samatta ukikatiza maeneo ya Morocco
Baadae akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na washabiki wa soka kama uonavyo pichani
Baadae akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na washabiki wa soka kama uonavyo pichani
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini,huku Nyota wetu Mbwana Samatta akiwa amepozi na tuzo yake ya mchezaji bora wa Afrika.
Samatta akipata picha ya pamoja na Waziri Mh.Nape Nnauye.
Wadau wa Soka wakijadiiana jambo,wakati huo Samatta anafanya mahojiano ya hapa na pale na baadhi ya vyombo vya habari
Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauyewakijumuika pamoja kwenye hafla fupi ya kumpongeza Mbwana Samatta ndani ya kiota cha maraha-Escape One Mikocheni jijini Dar
Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape na wadau wengine wa soka wakijumuika kwa pamoja kumpongeza Samatta.


Benzema alimalizia mpira uliomshinda Ronaldo na kufunga dakika ya 90 na mtanange kumalizika kwa bao 5-0 Real wakiibuka kidedea na kumwanzishia ushindi mnono meneja mpya Zinedine Zidane leo hii.
Kipindi cha pili dakika ya 49 Bale akapachika bao la tatu na kufanya matokeo kuwa 3-0 dhidi ya Deportivo L Coruna.

Benzema Dakika ya 15 na Bale dakika ya 22 tayari wameshaziona nyavu kipindi cha kwanza...hadi mapumziko 2-0.
VIKOSI:
REAL XI:
Navas, Carvajal, Ramos, Pepe, Marcelo, Modric, Kroos, Isco, Bale, Ronaldo, Benzema
DEPORTIVO XI: Lux, Navarro, Arribas, Sidnei, Fajr, Luis Alberto, Cartabia, Juanfran, Pedro Mosquera, Bergantinos, Lucas



Rooney akipiga penati na kumfunga kipa wa Sheffield United.
BAO la Penati ya Dakika ya 93 iliyofungwa na Kepteni Wayne Rooney imewaingiza Manchester United Raundi ya 4 ya FA CUP walipoitungua Timu ya Daraja la chini Sheffield United 1-0 Uwanjani Old Trafford.Penati hiyo ilitolewa katika Dakika ya 92 baada ya Memphis Depay, alieingizwa Kipindi cha Pili na kuleta uhai mkubwa kwenye mashambulizi, kumtambuka John Brayford na kuingia ndani ya Boksi na kuchezewa Rafu na Dean Hammond.
Bao hilo la Rooney lilileta ahueni kubwa kwa Man United kwani walitawala Mechi yote, kwa Asilimia 72 lakini walilenga Shuti 1 tu Golini dhidi ya Timu ya Daraja la chini ambayo iliamua kujihami.
Man United watajua wapinzani wanaofuatia baada ya Droo ya Raundi ya 4 ambayo itafanyika Jumatatu Usiku.

Wayne Rooney akimlalamikia bmwamuzi kuhusu rafu hiyo!Kipindi cha kwanza kilimalizika 0-0
BAADA ya kuanza poa 2016 kwa kuitwanga Swansea City 2-1 kwenye Ligi Kuu England, sasa Manchester United wako tena kwao Old Trafford kucheza Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP na Sheffield United inayocheza Daraja la chini, Ligi 1,ikiwa ni Madaraja Mawili chini ya Ligi Kuu England.
Man United wanaanza kampeni ya kulitwaa Kombe hili ambalo mara ya mwisho walilichukua Mwaka 2004, ikiwa ni mara yao ya 11, na wamepitwa tu na Arsenal waliolitwaa mara 12 baada ya kulibeba mara 2 mfululizo kwa Miaka Miwili iliyopita.


Mbele ya Mashabiki 70,720, Barcelona iliinyuka Granada Bao 4-0 kwa Bao 3 za Lionel Messi na 1 la Neymar, na kuchukua uongozi wa La Liga.
DAKIKA ya 58 kipindi cha pili dakika ya 58 na bao la nne lilifungwa na Staa mwingine Neymar dakika ya 83 na mtanange kumalizika 4-0 dhidi ya Granada. Lionel Messi kafunga yote mawili katika kipindi cha kwanza, Akifunga bao la kwanza dakika ya 8 na bao la pili akilifunga dakika ya 14 na kufanya Timu yakke kuwa mbele ya bao 2-0. Ushindi huu, ambao ni Mechi ya kiporo, umewaweka Barca kileleni wakiwa Pointi 1 mbele ya Atletico Madrid na Pointi 5 mbele ya Real huku zote zikicheza Mechi 18.


BAO za Arsenal zimefungwa na Joel Campbell dakika ya 25,  Aaron Ramsey dakika ya 72 na lile la  Olivier Giroud dakika ya  75 na mtanange kumalizika kwa bao 3-1 dhidi ya Sunderland.
BAO la Sunderland  limefungwa na Jeremain Lens dakika ya 17
1-1 na mpira kwenda mapumziko
Soma Zaidi Hapa »

waliotembelea blog