Rooney akipiga penati na kumfunga kipa wa Sheffield United.
BAO la Penati ya Dakika ya 93 iliyofungwa na Kepteni Wayne Rooney imewaingiza Manchester United Raundi ya 4 ya FA CUP walipoitungua Timu ya Daraja la chini Sheffield United 1-0 Uwanjani Old Trafford.
Bao hilo la Rooney lilileta ahueni kubwa kwa Man United kwani walitawala Mechi yote, kwa Asilimia 72 lakini walilenga Shuti 1 tu Golini dhidi ya Timu ya Daraja la chini ambayo iliamua kujihami.
Man United watajua wapinzani wanaofuatia baada ya Droo ya Raundi ya 4 ambayo itafanyika Jumatatu Usiku.
Man United wanaanza kampeni ya kulitwaa Kombe hili ambalo mara ya mwisho walilichukua Mwaka 2004, ikiwa ni mara yao ya 11, na wamepitwa tu na Arsenal waliolitwaa mara 12 baada ya kulibeba mara 2 mfululizo kwa Miaka Miwili iliyopita.
0 maoni:
Post a Comment