Msafara
wa magari uliokuwa umembeba Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika
wa Wachezaji wa Ndani 2015, Mbwana Samata,ulionaswa na Camera ya Globu
ya jamii maeneo ya Morocco jana jioni ukitokea hoteli ya Kempinsk baada
ya kuzungumza na vyombo vya habari,Msafara huo akiwemo Waziri wa
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye ulipita maeneo kadhaa
ya jiji la Dar na kukomea katika kiota cha Escape One Mikocheni jijini
Dar,ambako alikutana na kupongezwa na Wadau mbalimbali wa tasnia ya
Michezo.Mwanasoka huyo aliwasili juzi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam akitokea Abuja, Nigeria
katika hafla ya utoaji tuzo kwa mwanamichezo bora.
PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
Baadhi
ya Waendesha Boda boda nao hawakuwa na hiyana kuunga mkono mafanikio ya
Mbwana Samatta,ambayo yameiletea heshima kubwa nchi yetu.
Msafara wa Mbwana Samatta ukikatiza maeneo ya Morocco
Baadae
akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape
Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na
washabiki wa soka kama uonavyo pichani
Baadae
akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape
Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na
washabiki wa soka kama uonavyo pichani
Baadhi
ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini,huku Nyota wetu
Mbwana Samatta akiwa amepozi na tuzo yake ya mchezaji bora wa Afrika.
Samatta akipata picha ya pamoja na Waziri Mh.Nape Nnauye.
Wadau wa Soka wakijadiiana jambo,wakati huo Samatta anafanya mahojiano ya hapa na pale na baadhi ya vyombo vya habari
Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri
wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauyewakijumuika pamoja
kwenye hafla fupi ya kumpongeza Mbwana Samatta ndani ya kiota cha
maraha-Escape One Mikocheni jijini Dar
Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape na wadau wengine wa soka wakijumuika kwa pamoja kumpongeza Samatta.
0 maoni:
Post a Comment