
Sturridge,
Lallana, Johnson, Steven Gerrard, Rickie Lambert wote furaha wakti wa
Mazoezi kujiandaa na Mtanange wao kwao dhidi ya Man United.
Timu zote zinatinga kwenye Mechi hii
zikiwa kwenye fomu nzuri kwa Liverpool kushinda Mechi 5 mfululizo za
Ligi Kuu England na Man United kushinda Mechi 3 mfululizo zilizopita.
Baada
ya Liveroool kuchapwa 3-0 Uwanjani Old Trafford hapo Desemba 14 na Man
United na kuachwa Nafasi ya 10 kwenye Ligi, Liverpool, chini ya Meneja
Brendan Rodgers, hawajapoteza Mechi yeyote ya Ligi na sasa wapo Nafasi
ya 5 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Man United walio Nafasi ya 4.
Mshikamano..Wachezaji wa Liverpool wakifurahia

Lucas Leiva na Kolo Toure kwenye mazoezi leo hii

Kocha wa Liverpool akifurahia jambo wakati wa Mazoezi..
Wakati Brendan Rodgers akipooza umuhimu
wa Mechi hii ya Anfield na kudai bado zipo Mechi nyingi muhimu, Meneja
wa Man United Louis van Gaal ametoa msisitizo kwa Wachezaji wake
kudhibiti jazba hasa baada ya Timu yake kuathirika na Kadi Nyekundu
dhidi ya Timu kubwa na hilo kumfanya awe Refa kwenye Mechi za Mazoezi
ili kuwaonya Wachezaji wake.
Alipohojiwa kwa nini Kepteni wake Wayne
Rooney huwa hafungi Anfield ambako mara ya mwisho kupiga Bao ni karibu
Miaka 10 iliyopita, Van Gaal alisema ni kawaida kwa Mchezaji yeyote
lakini anaamini hilo halitamwathiri Rooney kucheza vyema.
Dejan

Aaaah

Lazar na Javier

Kolo Toure