Thursday, September 24, 2015


Stori za soka la wanawake kukua zimezidi kuchukua nafasi duniani kote ila kinachovutia ni kuwa utamaduni wa nchi za kiarabu ambazo zimekubali kuunga mkono soka la wanawake lakini kwa baadhi ya masharti kwa washiriki hao kama mavazi na mengineyo.
September 24 ninayo stori kutoka Iran inayohusu soka la wanawake, ambapo timu ya taifa ya Iran ya wanawake ambayo inashiriki michuano ya mpira wa miguu Nilai Malaysia, inashiriki mashindano hayo bila kuwa na nahodha wake Niloufar Ardalan, nahodha huyo hayupo na timu Malaysia kwa sababu mume wake amegoma kusaini nyaraka ili mkewe apate kibali cha kusafiri nje ya Iran.
mideast-iran-ardalan-310x415
Sheria ya nchi ya Iran hairuhusu mwanamke kusafiri nje ya nchi pasipo ruhusa ya mumewe, yaani hii ni tofauti kidogo na kwetu kwani tumezoea kuona wanawake wakikatazwa kufanya vitu flani na wame zao, lakini bado wana nafasi ya kuendelea kufanya kwani sio kosa kisheria kufanya maamuzi yako.
Kwa Iran mwanamke lazima mumewe asaini nyaraka rasmi ili mkewe aweze kusafiri nje ya nchi, hivyo nahodha wa timu hiyo ya Iran Niloufar Ardalan ameshindwa kusafiri kwenda Malaysia kwa sababu ya mumewe lakini hii ndio kauli yake.
201162673751812734_20
“Haya mashindano yalikuwa muhimu sana kwangu kama mwanamke wa kiislamu nilikuwa nataka kupeperusha bendera ya nchi yangu katika mashindano hayo na sio kusafiri kwa kujifurahisha, nafikiri mamlaka husika zingetengeneza sheria za kuwalinda wanamichezo wa kike hususani katika hali kama hi

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog