Kikosi cha Timu ya Wakata Miwa Kagera Sugar
wameanza leo hii safari kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa
ufunguzi wa Ligi kuu soka Tanzania bara katika uwanja wa CCM Mkwakwani
dhidi ya wenyeji Mgambo JKT, septemba 20 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa
Kagera Sugar, Murage Kabange amesema klabu hiyo ina jumla ya wachezaji
25 na hii leo tayari wapo safari na viongozi watano kwenda kusaka
pointi tatu muhimu.
Kabange aliongeza kuwa wameamua kuanza safari mapema kwasababu kutoka Kagera kwenda Tanga ni mbali sana..JPG)
Viongozi wa Kagera Sugar
.JPG)
Ubutu
wa safu ya ushambuliaji lilikuwa tatizo la kudumu kwa Kagera Sugar
lakini kwa sasa limepata marekebisho kwani wamesajili Vijana wa nguvu
msimu huu.
.JPG)
WAKATA
miwa wa Kaitaba, `Wanankulukumbi` Kagera Sugar wakijifua kwenye Uwanja
wa Kagera Sugar hivi karibuni tayari kwa Ligi kuu Vodacom sep 20 mwaka
huu. Kagera Sugar wataanza ufunguzi wa Ligi kuu Vodacom Ugenini na timu
ya Mgambo JKT mkwakwani Mjini Tanga wikiendi hii.
.JPG)
Kocha
huyo alisema: “Tuna imani na vijana wetu kuwa wanaweza kutufikisha
tunapotaka, japokuwa ligi ya msimu huu inaonekana itakuwa ngumu, lakini
tutajitahidi kupigana ili kuweza kushika nafasi za juu”.
.JPG)
Wachezaji wa Kagera Sugar wakifaya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Kaitaba Hivi karibuni.
.JPG)
Baadhi
ya Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa Uwanjani Kaitaba
wakishuhudia mazoezi ya Vijana wao. Wakijifua kujiandaa na Ligi Kuu
Vodacom msimu mpya 2014/15 inayotarajia kuanza hivi Karibuni sep.20
mwaka huu.
.JPG)
Murage
Kabange, kocha msaidizi wa Kagera Sugar (kulia) tayari amebainisha kuwa
mapungufu waliyokuwa nayo katika kikosi chao kuwa wameishayafanyia
marekebisho na wako tayari kupambana na Mgambo JKT ya Mjini Tanga.
.JPG)
Kocha
Mkuu wa Kagera Sugar (kulia) Bw. Jackson Mayanja akiangalia vijana wake
wakati w mazoezi yao kwenye Uwanja wao wa Nyumbani Kaitaba hivi
karibuni