Saturday, August 1, 2015


Kocha wa makipa wa Yanga SC, Juma Pondamali (kushoto) akiwa na mabosi wake, Charles Boniface Mkwasa (katikati) na Hans van der Pluijm (kulia) Jumatano wakati wa mchezo dhidi ya Azam FC
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
IMEZOELEKA Juma Pondamali ‘Mensah’ ni mchangamfu na mcheshi wakati wote, tangu anacheza.
Kipa huyo wa zamani wa kimataifa nchini aliyewika Yanga SC na Pan African- ambaye alipewa jina la utani Mensah enzi zake, alikuwa katika hali tofauti kabisa Jumatano wiki hii.
Katika siku ambayo Yanga SC ilitolewa na Azam FC kwa mikwaju ya penalti, Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Pondali alikuwa mnyonge tangu mwanzo.
Baada ya makocha wa Yanga SC kuingia uwanjani na kwenda kuketi katika benchi lao, Pondamali alikuwa mnyonge aliyeshika tama muda mwingi wakati mabosi wake, Mholanzi, Hans vand der Pluijm na mzalendo, Charles Boniface Mkwasa wakitafakari mchezo.
Dakika 90 za mchezo huo uliofanyika Jumatano jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zikamalizika kwa sare ya 0-0 na sheria ya mikwaju ya penalti ikachukua nafasi yake kuamua mshindi.
Makocha wote wa Yanga SC na wachezaji wa akiba waliungana na wenzao waliotoka uwanjani kuwapa ‘mawili matatu’ kuelekea kwenye matuta, lakini Pondamali hakuinuka kwenye benchi.
Mkwasa akimuelekeza Barthez namna ya kudaka penalti
Dida akimuandaa Barthez kwenda kudaka penalti

Ikabidi kazi ya kumuandaa kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ kuelekea kwenye matuta ifanywe na kipa mwenzake, Deo Munishi ‘Dida’. Na baadaye, kocha Mkwasa akamuita Barthez na kuanza kumpa maelekezo namna ya kucheza penalti.
Mkwasa hajawahi hata kuwa kipa, enzi zake alikuwa beki na kiungo- lakini akawa anamuelekeza Barthez namna ya kudaka penalti.
Hata wakati wa dua ya kabla ya wachezaji wa Yanga SC kurudi uwanjani kwa ajili ya penalti, Pondamai aliinuka mwishoni kabisa kwenda kujiunga na mduara.
Hakuwa katika hali ya kawaida Pondamali, kama ambavyo amezoeleka, mchangamfu na mcheshi muda mwingi.
Barthez akaenda kutunguliwa penalti zote tano na Mwinyi Hajji Mngwali akakosa penalti moja ya Yanga, Azam FC ikasonga mbele kwa ushindi wa penalti 5-3. Nini kilikuwa kimemsibu Pondamali siku hiyo?

Dua ya kuelekea kwenye penalti imeanza, lakini Pondamali hajajiunga na mduara
  
Pondamali (kushoto) alitokea mwishoni kabisa kujiunga na mduara wa dua
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole kujihusisha na shughuli za sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.
Mwanamuziki huyo anayejulikana pia kama Shishi Baby amekumbwa na dhahama hiyo baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha akicheza jukwaani akiwa katika mavazi yanayokinzana na maadili ya Kitanzania akiwa nchini Ubelgiji.

Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza amezungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu leo na kusema hatua hiyo imechukuliwa baada ya awali kumpa onyo kwa matukio ya kupanda jukwaani kufanya sanaa akiwa katika mavazi yasiyozingatia maadili ya Kitanzania.
“Awali tulimuonya kwa vitendo hivi, akakiri kosa na kuahidi kwa maandishi kuwa hatarudia kufanya hivyo” alisema na kuongeza: “Hata hivyo, wadau wa muziki watakumbuka alichokifanya nchini Ubelgiji. Lilikuwa tukio la aibu kwake kama msanii, aibu kama mwanamke na aibu kama Mtanzania” alisema.
Amewataka wasanii kujitathimini kabla ya kupanda jukwaani na kuonya kuwa Basata itaendelea kuchukua hatua kama hizo dhidi ya msanii yeyote atakayebainika kuvunja/kukiuka maadili ya nchi. Shilole amekiri kupokea barua kutoka Basata akisema, hivi sasa yuko kwenye majadiliano na mwanasheria wake na kusema anakusudia kukata rufaa kupinga kufungiwa huko. “Mashabiki wangu watulie kwani hii ni changamoto, tunaifanyia kazi kila kitu kitakuwa sawa hivi karibuni” alisema.


Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
IKITAJWA orodha ya wachezaji waliong’ara katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na jina la winga wa kushoto wa Azam FC, Farid Malik Mussa (pichani kulia) likakosekana itakuwa kuna mushkeli.
Farid ameng’ara Kagame ya 2015 inayofikia tamati kesho Dar es Salaam na amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake kufika Fainali, ambako itamenyana na Gor Mahia ya Kenya.
Maamuzi ya Kocha Muingereza Stewart Hall, kutowaorodhesha kwenye kikosi cha Kagame mawinga Brian Majwega na Ramadhani Singano ‘Messi’ yalipata upinzani ndani ya uongozi wa Azam FC awali.
Lakini sasa yamekuwa maamuzi ambayo yameleta faraja kwenye timu, kwani dogo aliyepandishwa kutoka akademi ya Azam FC mwaka juzi, Farid amefanya watu wasahau kwa muda kuhusu Majwega na Messi.
Farid amecheza vizuri kule kushoto na amekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia timu kupata mabao kabla ya kufunga bao pekee la ushindi katika mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya KCCA jana. 
Na ukitazama wachezaji wa kushoto wa timu nyingine zilizoshiriki mashindano haya hadi sasa, anaweza akapatikana wa kumzidi Farid kwa urefu, mwili na umri- lakini si uwezo.
Farid Mussa akimuacha chini beki wa Yanga SC, Juma Abdul katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Kagame

 

Farid ameonyesha uwezo mkubwa katika mashindano haya hadi sasa, kasi yake, uwezo wa kumiliki mpira, kupiga chenga, akili na maarifa ambayo yanamfanya awe na maamuzi sahihi wakati wote.
Si winga ‘mambio akili sifuri’ kama mawinga wetu wengi wa sasa nchini, huyu ni ‘winga maujuzi’, ambaye anapomtoroka beki anafahamu anakwenda wapi na akifika hapo atafanya nini.
Farid anamchukua beki anamburuza, akifika karibu na kona anainua shingo anaangalia pale ndani wenzake wamekaa vipi, akiona hawajajipanga vizuri, anaingia ndani zaidi kuwavuta.
Ndiyo sababu krosi zake nyingi husaidia Azam FC kupata bao au kusababisha kizaazaa kwenye lango la wapinzani.
Farid kwa sasa ni tishio kwa mabeki na wachezaji mbalimbali wamemzungumzia kama winga bora wa Kagame 2015.
Kesho Saa 10:00 jioni Kombe la Kagame litafikia tamati kwa mchezo wa Fainali kati ya Azam FC na Gor Mahia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Bila shaka itakuwa ni siku nyingine ya kuendelea kushuhudia ubora wa Farid.

Ameposti kwenye Twitter picha hii
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Theo Walcott amesaini Mkataba mpya wa miaka minne kuendelea kuichezea Arsenal.
Katika Mkataba huo mpya, Walacott anaingia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi kwenye klabu hiyo.
Mpachika mabao huyo wa England sasa atakuwa anaingiziwa kwenye akaunti yake benki Pauni 140,000 kila wiki sambambaa na nyota wengine wa The Gunners akina Alexis Sanchez na Mesut Ozil.
Walcott, ambaye ndiye mchezaji wa muda mrefu zaidi Arsenal alikuwa anasumbuliwa na majeruhi msimu uliopita, lakini kwa sasa yuko fiti na alifunga bao pekee la ushindi dhidi ya Wolfsburg wikiendi iliyopita katika Kombe la Emirates.
Theo Walcott celebrated his new Arsenal contract in snaps taken by club photographer Stuart MacFarlane
Theo Walcott amefurahia Mkataba wake mpya Arsenal kwa kuweka picha hizi zilizopigwa na mopiga picha wa klabu, Stuart MacFarlane

Walcott celebrates with the Emirates Cup after scoring the winner against Wolfsburg last Sunday


Luke Shaw pictured in Manchester United's new adidas kit in Sportsmail's exclusive photograph after their £750million mega-deal

Juan Mata, new signing Bastian Schweinsteiger and Ander Herrera pose in the club's new adidas kit after 13 seasons with Nike

Herrera, Mata and Phil Jones were among the United players taking part in the launch of the club's new kit for the 2015/16 season

Daley Blind poses in the first kit made by German sportswear giants adidas after they signed a £750m world record deal with the club

Team-mates Young, Mata and Blind pose together in the new United kit sponsored by adidas which was unveiled at midnight


MANCHESTER UNITED BEI ZAKE
Short sleeve shirt - £60
Short sleeve shirt (kids) - £50
Short sleeve shirt (women's) - £55
Shorts - £25
Shorts (kids) - £20
Socks (black or white) - £12
Full home kit (shirt, shorts, socks) - £97


James Wilson poses in the newly-released retro-looking kit which may have some United supporters thinking back to the 80s and 90s
The kit went on sale at selected locations in Manchester and London at midnight, and was launched by Daley Blind and Phil Jones


 NGAO YA Jamii huko England ndio Mechi ya fungua dimba Msimu mpya na hushindaniwa kati ya Mabingwa Watetezi wa England na waliobeba FA CUP na safari hii Mabingwa Chelsea wataivaa Arsenal ambao walitwaa FA CUP Msimu uliopita.
Wakati Arsenal wakitinga kwenye mtanange huo wakiwa na matokeo mazuri kwenye Mechi zao za kabla ya Msimu za kugombea Barclays Asia Trophy huko Singapore na Emirates Cup Uwanjani kwao Emirates Jijini London na kubeba Makombe yote, Mabingwa Chelsea wao hawajashinda hata Mechi moja, ndani ya Dakika 90, katika Mechi zao za matayarisho.
Katika Mechi hizo, Arsenal walipata ushindi mkubwa pale walipoichapa Lyon ya France 6-0 Uwanjani Emirates na pia kuitwanga Everton 3-1 huko Singapore.
Katika Mechi zao 4 za majaribio, Arsenal wameona nyavu mara 14 na kufungwa mara 1 tu huku Kipa Mkongwe, Petr Cech, waliemnunua toka Chelsea aking’ara.
Cech anaweza kukutana na Timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza Jumapili hii ikiwa atapangwa wakati Arsenal wakisaka kutwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya pili mfululizo kwa mara ya kwanza tangu 1999.
Wakati Arsenal wakibembea kuelekea Mechi hii ya Ngao ya Jamii ambayo Msimu uliopita waliitwanga Manchester City 3-0 na kuibeba, Chelsea wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa hawajashinda ndani ya Dakika 90 baada ya kuhitaji Tombola ya Penati kuzibwaga PSG na Barcelona kufuatia kuchapwa 4-2 na New York Red Bulls kwenye Mashindano ya International Champions Cup huko Marekani.
Mbali ya hayo, Chelsea pia hawana Rekodi nzuri ya kutwaa Nagao ya Jamii baada ya kuitwaa mara 4, mara ya mwisho ikiwa 2009, wakati Arsenal wameibeba mara 13 wakipitwa tu na Liverpool waliotwaa mara 15 na vinara Manchester United ambayo imeichukua mara 20.

Mourinho akiteta jambo na Terry na  Fabregas pamoja na wengine

Wachezaji wa Chelsea wamejifua leo Ijumaa tayari kwa kipute jumapili
Chelsea kukutana na Washindi wa  FA Cup  Arsenal kwenye  Community Shield  huko  Wembley siku ya jumapili

Kikosi cha Timu ya Black Sailor iliopanda daraja mwaka huu kucheza Ligi Kuu ya Zanzibar kwa Msimu wa mwakac 2015/2016, ilikubali kupigo cha mabao 4--0 dhidi ya timu ya Simba katika mchezo wa kirafiki uliofanyika usiku huu katika uwanja wa amaan Zanzibar.

Kikosi cha Simba kilichotoa kipigo kwa Timu ya Black Sailor uwanja wa Amani usiku huu Simba ikiwa Zanzibar kwa michezo ya kirafiki kuimarisha Kikosi chake kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.

Jopo la Makocha wa timu ya Simba wakifuatilia mchezo huo wa kirafiki na timu ya Black Sailor

Mchezaji wa timu ya Simba akikokota mpira akijiandaa kumpita beki wa timu ya Black Sailor, wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Simba imeshinda 4-0

Mchezaji wa timu ya Black Sailor akiwapita wachezaji wa timu ya Simba katika mchezo wa kirafiki.

Mshambuliaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Black Sailor


Mchezaji wa timu ya Simba Abdi Banda akiifungia timu yake bao la kwanza kwa kichwa katika mchezo huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya Simba imeshinda bao 4--0

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na mchezaji Abdi Banda kwa kichwa baada ya kupigwa krosi na Khamis Kiiza, mwenye jezi namba 5

Mshambuliaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Black Sailor wakati wa mchezo wao wa kirafiki.

Mshambuliaji wa timu ya Simba Khamis Kiiza akimpita beki wa timu ya Black Sailor


Thomas Bach akitangaza mshindi wa kura ya uwenyeji wa Olimpiki ya msimu wa baridi 2022
Mji mkuu wa Beijing ndio utakaokuwa mwenyeji wa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi ya mwaka wa 2022.
Mji huo wa China umeipiku mji pinzani wa Almaty ulioko Kazakhstan .
Beijing ambayo iliandaa mashindano ya Olimpiki ya mwaka wa 2008 ya msimu wa joto sasa umeingia katika daftari za kihistoria kwa kuwa mji mkuu wa kwanza kuandaa mashindano yote mawili ya Olimipiki ya msimu wa joto na yale ya msimu wa Baridi.
Kamati kuu ya kimataifa ya Olimpiki, ilikuwa ikikutana Kuala Lumpur,kupiga kura ya kuchagua mji upi kati ya Beijing au Almaty itakuwa mwenyeji wa mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi mnamo mwaka 2022.
Ripoti kutoka Kuala Lumpur, mahala ambapo uamuzi huo umetolewa, inasema kwamba kamati hiyo ya IOC, iliamua kupiga kura kwa kutumia makaratasi baada ya kutokea matatizo ya kimitambo, katika shughuli za upigaji kura kielektroniki.
Mji huo mkuu wa China ni eneo zuri kwani lina uzoefu wa muda mrefu hasa baada ya kuandaa mashindano ya Olimpiki ya majira ya joto, mnamo mwaka 2008. Wawakilishi wa Beijing wakijipigia debe
Beijing ilikuwa ikijipigia debe ikisema kuwa kukosekana kwa barafu hakutakuwa na tatizo lolote.
Nao mji wa Almaty, nchini Kazakhastan, ulikuwa unaiomba kamati hiyo kuu ya kimataifa ya Olimpiki, kufanya maamuzi ya kina na kupigia kura jiji ambalo lenye barafu nyingi ardhini.

waliotembelea blog