Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
Bara 2014- 2015, Yanga wakishangilia ubingwa wao huo mara baada ya
kumalizika kwa mtanange wao dhidi ya Azam FC, uliopigwa kwenye Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Mtanange huo ulimalizika kwa Azam FC
kushinda Bao 2-1. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, MMG. 
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi Nahodha wa Timu ya
Yanga, Nadir Haroub cheti cha pongezi kutoka kwa Rais wa Shirikisho la
Soka Duniani, Sepp Blatter kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania
Bara 2014 - 2015.Kushoto ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wa pili kulia
ni Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji.
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza Mshambuliaji wa Yanga,
Mrisho Ngassa baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji bora wa mwezi wa nne.
Wachezaji wa Timu ya Yanga wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na
timu ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Mwali kabla ya kukabidhiwa kwa wenyewe.
Watu wa huduma ya kwanza wakifatilia mchezo huku wakiangalia yule
atakaeumia na kwenda kumsaidia, hii ni kutokana na Mvua kubwa
inayoendelea kunyesha hapa jijini Dar leo.
Nyanda wa Timu ya Azam, Mwadini Ali akiwa makini kulinda wakati mashambulizi yakiandama upande huo.
Msambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (kulia) akimkimbiza Kiungo wa Kati
wa Azam, Mudathir Yahya wakati wa mtanange wa ligi kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar. Azam imeshinda bao 2-1.