
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma
alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo
zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa
chama hicho.
Aidha, amesema
kuwa vita aliyopo siyo kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu
wengi, akitaja magenge ya watu wanaotaka urais 2015 na walioficha fedha
nje ya nchi walioungana...