Tuesday, September 23, 2014

Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini...
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam MBEYA City fc imepata pigo baada ya wachezaji wake watatu kuumia katika mechi ya jumamosi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu  iliyomalizika kwa suluhu ya bila kufungana, uwanja wa Sokoine, Mbeya, na watakaa nje ya uwanja kwa wiki mbili. Afisa habari wa klabu hiyo, Dismas Ten ameiambia MPENJA BLOG mchana huo kuwa baada ya mechi iliyopita, wachezaji watano...
Na Baraka Mpenja, Dar esl salaam IMEELEZWA kuwa mshambuliaji wa Simba sc, Mkenya Paul Kiongera Mungai leo amefanyiwa vipimo hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia kuumia goti katika sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union, jumapili iliyopita uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Katika vipimo vya awali, Kiongera amebainika kuwa na majeruhi sugu ya goti kama ilivyowahi kuelezwa na mtandao...
Aliyekuwa Rais wa TFF, Leodigar Chila Tenga alikuwa mchezaji muhimu wa Taifa Stars miaka ya 1980 HISTORIA inaonesha kuwa zamani mpira wa miguu ulikuwa unachezwa kutoka ngazi ya chini mpaka juu na walipatikana wachezaji wengi wa kulisaidia taifa. Taifa Stars iliyoshiriki michuano ya mataifa ya Afrika nchini Nigeria miaka ya 1980, ni ushahidi tosha juu ya suala hilo. Katika kipindi hicho...
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) septemba 19 mwaka huu lilitangaza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa zilizoandikwa kwenye baadhi ya Vyombo vya Habari zikielezea tuhuma za hujuma kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mechi za kufuzu mashindano ya AFCON. Taarifa hiyo ilifafanua kuwa TFF pamoja na kutokuwa na uthibitisho wa tuhuma hizi nzito haliwezi kuzikalia kimya na...

waliotembelea blog