Monday, January 16, 2017
1:26 AM
Unknown
1:24 AM
Unknown
EVERTON Leo huko Goodison Park imewaonyesha Manchester City kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, kwa kuwatandika Bao 4-0 kipigo ambacho ni kibaya mno kwa Meneja wa City katika himaya yake kwenye Mechi za Ligi.
City walikuwa nyuma 1-0 hadi Haftaimu kwa Bao la Romelu Lukaku la Dakika ya 34.
Kipindi cha Pili Everton wakatandika Bao nyingine 3 katika Dakika 47, 79 na 90 Wafungaji wakiwa Kevin Mirallas na Chipukizi Tom Davies na Ademola Lookman.
Matoke ohayo yamewaacha City wakiwa Nafasi ya 5 na Everton wakiwa Nafasi ya 7.
Mechi inayofuata kwa City ni Jumamosi ijayo wakiwa kwao Etihad kucheza na Timu ngumu Tottenham Hotspur wakati Everton wako Ugenini huko Selhurst Park kucheza na Crystal Palace.
VIKOSI VILIVYOANZA:
EVERTON: Robles, Holgate, Ashley Williams, Funes Mori, Coleman, Davies, Barry, Baines, Barkley, Mirallas, Lukaku
Akiba: Schneiderlin, Jagielka, Lennon, McCarthy, Valencia, Stekelenburg, Lookman.
MAN CITY: Bravo, Sagna, Otamendi, Stones, Clichy, Zabaleta, Touré, Silva, De Bruyne, Sterling, Agüero
Akiba: Kolarov, Caballero, Jesus Navas, Delph, Sané, Iheanacho, GarcÃa.
1:23 AM
Unknown
Hii ni Mechi ya Mahasimu wakubwa Kihistoria huko England, waliocheza Mechi yao ya kwanza kabisa Tarehe 28 Aprili 1894 wakati huo Manchester United ikiwa na Jina lake la mwanzo kabisa Newton Heath, Mechi ambayo ilibatizwa ‘Dabi ya Kaskazini-Magharibi’ ikizikutanisha Timu zinazotoka Miji Miwili tofauti, Manchester na Liverpool.
Rio ameeleza zaidi: “Nadhani tunao Mameneja Bora Duniani hapa kwenye Ligi Kuu. Ukiwaondoa, pengine, Carlo Ancelotti, Diego Simeone na Zinedine Zidane, pengine tunao Bora hapa, wanaofurahisha na wenye hulka kubwa. Jose Mourinho ni mmoja wao na Jurgen Klopp pia ameleta msisimko mpya England!”
Kuhusu Klopp, Rio ametamka: “Jinsi anavyoisuka Timu yake Liverpool, inasisimua. Ni watamu kuwaangalia. Wanacheza kwa ari, wako moja kwa moja, wakishambulia kwa nguvu na wingi. Achilia mbali Klabu unayosapoti, Liverpool, chini ya Klopp, ni Timu nzuri kuitazama na hilo huwafanya wawe hatari. Wanashinda Gemu 3-2 au 4-3 na hio inaonyesha udhaifu wao kwenye Difensi lakini wakifunga zaidi ya Wapinzani wao basi watakuwa tishio kubwa!”
Ameendelea: “Wakinasa Mpira na Carrick akipokea Mpira, hatoi pasi ya upande, yeye atapenyeza mbele na kuvuka Viungo kufikia Mafowadi wake. Wachezaji wetu hatari ni Mafowadi na wanahitaji kupokea Mipira mapema. Kwa Miaka michache iliyopita tulikuwa tunacheza polepole na ilikuwa ngumu kuvunja ukuta wa Mtu 8 waliojipanga safu ya Mtu 4, Mtu 4. Hiyo ngumu kuwavunja lakini Carrick akicheza, akipata Mpira, yeye anapenyeza kuvuka ukuta huo na Mafowadi wetu wanapata nafasi za kupiga Mashuti. Magoli hufungwa hivyo. Yeye ni muhimu mno kwa sasa na kwa mbinu za Mourinho!”
“Kitu kingine muhimu kilichosaidia United kuwa bora zaidi ni kupanda kwa fomu za Wachezaji wao wapya Pogba, Mkhitaryan na Ibrahimovic. Hawa ni Mastaa wa Dunia. Na sasa tumerudi kusaini Mastaa wakubwa na si kama mwanzo. Akiwepo Mourinho, ni suala la muda tu na mambo yatakuwa safi. Kwa hili wimbi la sasa la mafanikio, kufuzu 4 Bora ni kitu kinachowezekana. Chochote zaidi ya hapo kitakuwa kitu kikubwa mno lakini kwangu kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI ndio lengo!”
Rio amesema zaidi: “Kwa haya, Mechi ya Wikiendi hii inakuwa kubwa zaidi kwa umuhimu wake. Siku zote Mechi hii ni kubwa lakini ukiangalia malengo ya Timu hizi, vipaji vya Wachezaji wao na ubora wa Mameneja wao, ni Gemu ambayo ni kubwa mno!”
JE WAJUA?
Uso kwa Uso:-Man United wameifunga Liverpool Mechi 79, Sare 53 na Kufungwa 65.
-Man United wametwaa Ubingwa wa England mara 20, mara ya mwisho ikiwa Mwaka 2013.
-Liverpool wametwaa Ubingwa wa England mara 18, mara ya mwisho ikiwa Mwaka 1990
Subscribe to:
Comments (Atom)
RSS Feed
Twitter