
LEO
Jumatano Mabingwa Watetezi wa UEFA CHAMPIONS LIGI Real Madrid wanarudi
tena Veltins-Arena, Mjini Gelsenkirchen huko Germany ambako Msimu
uliopita kwenye hatua kama hii ya Mashindano haya haya Real iliwanyuka
Wenyeji wao Schalke 6-1. Hata
hivyo safari hii Schalke wako chini ya Meneja wa zamani wa Chelsea
aliewabebesha Kombe hili Mwaka 2012 Roberto Di Matteo lakini wana
kibarua kigumu...