Monday, July 20, 2015

Vipindi vya Bongo Star search vimeanza kwenda hewani, na siku ya jana imeruka episode ya kwanza kuonyesha mchujo jinsi ulivyoenda mpaka kubakiwa na Top 6 (pichani) ya washiriki kutoka Mwanza ambayo itajumuika na washindi wa mikoa iliyosalia. Kipindi kitakuwa kinaruka kila siku ya Jumapili, saa tatu kamili kwenye vituo vya televisheni vya Clouds Tv na Star Tv na marudio yake; Kwa Clouds...
Usajili wa kipa Mhispania David De Gea kuelekea klabu ya Real Madrid kwa sasa inaonekana kama huenda usitokee tena hivi karibuni baada ya klabu hii ya Hispania na wenzao wa Manchester United kushindwa kufikia makubaliano . Manchester United imegoma kabisa kufanya mazungumzo na Real kuhusiana na De Gea kutokana na Wahispania hao kushindwa kutimiza masharti ambayo United imeyaweka katika...
Ikiwa imepita miezi miwili tangu rais wa Fifa Sepp Blatter alipotangaza kuiacha wazi nafasi yake baada ya  kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Fifa , shirikisho hilo limetangaza tarehe ya uchaguzi wake mkuu utakaofanyika kujaza nafasi ya Blatter. Uchaguzi huo sasa utafanyika tarehe 26 mwezi Februari mwaka 2016 kwenye makao makuu ya Fifa huko nchini Uswisi...
Taarifa za usajili ndio kitu ambacho kimekuwa kikitengeneza headlines nyingi kwenye vyanzo vya taarifa za kimichezo hususan mchezo wa soka barani ulaya na mojawapo kati ya taarifa ambazo leo (alhamis) zimeonekana kuwavuta wengi ni hii hapa . Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamefikia makubaliano na klabu ya Juventus juu ya usajili wa kiungo hodari raia wa Chile Arturo Vidal ambapo...
Bado kuna hali ya sintofahamu miongoni mwa uhusiano uliopo kati ya Shilole na Nuhu Mziwanda. Shilole amesema kwa sasa wamegombana na hatarajii kuachia wimbo na mwenzake huyo ambaye walipanga kutoa wimbo..amesema mtu akizungua na yeye anamzingua.. Amesema Nuhu amekua na wivu sana wakati yeye anaangaika kutafuta pesa..ila amesema akijua alipokosea...
Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amezoeleka kuwa aina ya kocha ambaye hapendi masikhara toka kwa wachezaji wake na amekuwa si mzito kufanya maamuzi ya kumuondoa mtu kwenye timu pale ambapo anaona anakwenda kinyume na matarajio yake . Hilo lilidhihirika siku chache zilizopita wakati ambapo kocha huyo alipotangaza wazi kuwa na mpango wa kumuuza kipa namba mbili Victor Valdez kutokana...
KIPA wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Mwameja Mohamed Mwameja aliyewika Simba SC, amesema kwamba ukipa si ‘lele mama’. Mwameja aliyewahi pia kudakia Ndovu ya Arusha na Coastal Union ya Tanga, amewataka makipa kujituma na kuzingatia nidhamu kwenye fani hiyo ili kufikia mafanikio. Mwameja ambaye alipewa jina la Tanzania One kwa umahiri wake wa kusimama imara langoni amekiri kuwa kuna magolikipa...

waliotembelea blog