Friday, April 3, 2015


\
 Nyakwesy Mujaya akimpa au mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi.

Msama akipeana mkono na Ifeanyi Kelechi.

NA LOVENESS BERNARD
MWIMBAJI wa kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka nchini
Uingereza, Ifeanyi Kelechi, ametua nchini kwa ajili ya kutumbuiza katika
Tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, siku ya jumapili.



Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) ijumaa ya tarehe 10, Aprili mwaka huu, itashuka dimbani Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakarisbisha timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (The She-Polopolo).

Twiga Stars inayonolewa na kocha mkuu Rogasian Kaijage iliingia kambini mwishoni mwa wiki na kikosi cha wachezaji 25 katika hostel za TFF zilizopo Karume, kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu wa kuwania kufuzu kwa fainali za michezo ya Afrika mwaka huu.


Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Lusaka Zambia, Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, mabao yaliyofungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).


Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kendelea kutimua vumbi mwishoni mwa wiki katika sita nchini, kwa michezo minne kucheza siku ya jumamosi na michezo mwiwili kuchezwa siku ya jumapili.
Jumamosi uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Simba SC kutoka jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Coastal Union wakiwakaribisha maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Ndanda FC ya Mtwara watakuwa wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika uwanja wa Nagwanda Sijaona, wakati maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatin uliopo Mlandizi.

Siku ya jumapili Stand United watawakaribisha wakata miwa kutoka Morogoro Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Polisi Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.



Olivier Giroud na Meneja  Arsene Wenger wamepewa Tuzo waote wawili huku Giroud akiwa mchezaji bora wa Premier League na Wenger kuwa Kocha Bora wa Mwezi huo wa Tatu.


Straika wa Arsenal Olivier  Giroud amefunga bao tano katika mechi alizocheza mwezi uliopita wa tatu

Wenger anapigana kucheza LIGI ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions)  msimu huu au kupanda juu

Arsenal wako nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu  Premier League kutokana na kushinda mechi zao za mwezi wa tatu na wako nyuma ya pointi 7 ya Chelsea.


USHINDI WA ARSENAL KWA MEZI WA TATU.
March 1 Arsenal 2-0 Everton (1 Giroud goal)
March 4 QPR 1-2 Arsenal (1)
March 14 Arsenal 3-0 West Ham (1)
March 21 Newcastle United 1-2 Arsenal (2)
Giroud analingana na Harry Kane kwa mabao kwa kwezi huo wa tatu lakini wanazidiana kitimu....Arsenal wameshinda mechi zote na Spurs wamefungwa mechi mbili za huo mwezi.

 

Raheem Sterling na Daniel Sturridge wakifurahia jambo wakati wa mazoezi kujiandaa na Mtanange wa Ligi Kuu England kati yake na Arsenal.

 
 Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers nae amesema mchezaji huyo kubaki Liverpool, Haendi kokote!! Bosi wa Brendan Rodgers amesema Fowadi wa Liverpool Raheem Sterling hataondoka mwishoni mwa Msimu licha ya mazungumzo ya Mkataba mpya kati yake na Klabu kuvunjika.
Juzi Sterling, Kijana wa Miaka 21, akifanya Mahojiano na BBC, alisema kuukataa Mkataba mpya ambao ungemlipa Pauni 100,000 kwa Wiki badala ya 35,000 za sasa si uroho wa Fedha Bali nia yake yeye na kutwaa Mataji.
Zipo ripoti kuwa Sterling yuko mbioni kuhamia Barcelona au Real Madrid Klabu za Spain lakini pia habari hizo zimegusia kubaki kwake England Ila atahamia Chelsea au Arsenal.
Mario nae alikuwemo mazoeziniMazoezi yakiendelea...Hapo Jana Brendan Rodgers amesema: "Liverpool no Mona ya Supapawa za Soka. Wamiliki wakisema hauzwi Mchezaji, basi hauzwi!"
Katika Mkataba wake was sasa na Liverpool, Sterling amebakisha Miaka Miwili.
Rodgers pia alisema Raheem, ambae alijiunga na Liverpool 2010 akitokea QPR, hakuruhusiwa kufanya Mahojiano na BBC lakini atajifunza kutokana na makosa take.

Pia Wachambuzi wengi was Soka huko Uingereza wameibuka na kumtaka Sterling abakie Liverpool kwani hajakomaa Kisoka kwenda nje.

waliotembelea blog