2-0 Wolverhampton Wanderers wanaongoza dhidi LiverpoolLiverpool
bado wako nyuma ya bao 1-0. Wolverhampton Wanderers tayari wanaongoza
bao dhidi ya Liverpool kwa bao la dakika ya 1 la Richard Stearm...
Saturday, January 28, 2017


MENEJA
wa Arsenal Arsene Wenger amefungiwa Mechi 4 na kutwangwa Faini ya Pauni
25,000 na FA, Chama cha Soka England, kwa Kosa la Utovu wa Nidhamu
alipopatikana na hatia ya kumkashifu Refa na pia kumsukuma Refa
Msaidizi. Wenger, mwenye Miaka 67, alimsukuma Refa Msaidizi
Anthony Taylor baada ya Refa wa Mechi yao na Burnley Jon Moss kumuamuru
kutoka Uwanjani kwa kutoa Lugha chafu. Kifungo...


RAUNDI ya 4 ya Kombe Kongwe Duniani, FA CUP,
imeanza kwa Sare ya 2-2 wakati Timu ya Daraja la chini Derby County
ikiwa Nyumbani kwao ilipowavaa Mabingwa wa England Leicester City. Wakiwa
nyuma kwa Bao 2-1, Leicester walinusurika kichapo baada ya Kepteni wao
Wes Morgan kusawazisha Dakika ya 86 na sasa Mechi hii itarudiwa huko
King Power Stadium Nyumbani kwa Mabingwa hao wa England ili kupata...


MECHI
za Robo Fainakli za AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika, zitaanza Jumamosi Januari 29 kwa Mechi 2 kati ya
Burkina Faso na Tunisia na kufuatia ile ya Senegal na Cameroon. Kati
ya hizo Mechi mbili ile ya Senegal na Cameroon ndio yenye mvuto na
mashamsham hasa baada ya Senegal kucheza vizuri mno kwenye Mechi zao za
Kundi B kwa kuzifunga Zimbabwe na...


Beki wa Sunderland Papy Djilobodji amefungiwa Mechi 4 baada ya kukutwa na hatia ya kucheza kwa fujo. Beki
huyo mwenye Miaka 28 alipinga Kosa lake ilipodaiwa alimpiga Usoni kwa
Mkono Mchezaji wa West Bromwich Albion Darren Fletcher wakati Timu yake
ikichapwa 2-0 Jumamosi iliyopita kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England. Tukio
hilo halikuonwa na Waamuzi wa Mechi hiyo na kupitiwa na Jopo Huru...



Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli kwa kuridhia
kufunguliwa tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kadhalika, TFF
inamshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
kwa juhudi zake na kwamba namna aliyoonesha ushirikiano kufanikisha
suala la kufunguliwa uwanja huo uliofungiwa...


BEKI
wa Sunderland Patrick van Aanholt anafanyiwa upimwaji Afya yake huko
Crystal Palace baada Klabu hizo mbili kuafikiana Dili inayotegemewa
kufikia Pauni Milioni 14. Beki huyo wa Kimataifa wa Netherlands
mwenye Miaka 26 ataungana tena na Bosi wa Palace Sam Allardyce ambae
walikuwa nae wote Sunderland. Van Aanholt alianza kuchezea Chelsea
lakini akapelekwa kucheza nje kwa Mkopo kewenye...


Kwa
mara nyingine tena Refa Jon Moss amemkwaruza Meneja wa Manchester
United Jose Mourinho baada ya maamuzi yake kwenye Mechi ya Pili ya Nusu
Fainali ya EFL CUP hapo Jana kumkera Mreno huyo wakati Hull City
ikiifunga Man United 2-1. Licha ya kipigo hicho, Man United
imetinga Fainali ya EFL CUP baada ya kuifunga Hull City 2-0 katika Mechi
ya kwanza na hivyo kusonga kwa Jumla ya Mabao 3-2...


LIGI DARAJA LA KWANZA
Mechi namba 34 (Pamba vs Friends Rangers). Kamishna wa mechi hiyo
Mnenge Suluja amepewa Onyo Kali kwa kutoripoti kitendo cha timu ya Pamba
kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) ikiwa na
wawakilishi watatu badala ya wanne. Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni
ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Mechi namba 35 (Kiluvya United
vs Lipuli). Timu ya Lipuli imepewa Onyo Kali kwa kuhudhuria kikao cha
maandalizi ya mechi (pre match meeting) ikiwa...
Subscribe to:
Posts (Atom)