RAUNDI ya 4 ya Kombe Kongwe Duniani, FA CUP,
imeanza kwa Sare ya 2-2 wakati Timu ya Daraja la chini Derby County
ikiwa Nyumbani kwao ilipowavaa Mabingwa wa England Leicester City.
Wakiwa nyuma kwa Bao 2-1, Leicester walinusurika kichapo baada ya Kepteni wao Wes Morgan kusawazisha Dakika ya 86 na sasa Mechi hii itarudiwa huko King Power Stadium Nyumbani kwa Mabingwa hao wa England ili kupata Mshindi.
Leicester walitangulia kufunga Dakika ya 8 baada Darren Bent kujifunga mwenyewe lakini Bent ndie alieisawazishia Bao Derby Dakika ya 21 na kwenda mbele 2-1 katika Dakika ya 40 kwa Bao la Craig Bryson.
Leo, Jumamosi zipo Mecho 10 na Jumapili zipo 5 ikiwemo ile ya kule Old Trafford kati ya Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Manchester United na Wigan Athletic.
Baadhi ya Mechi za Jumamosi ni ile ya kule Stamford Bridge wakati Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea wakicheza na Timu ya Daraja la chini Brentford.
Siku hiyo hiyo, Vigogo wa England Liverpool, ambao Raundi iliyopita walilazimika kucheza Mechi mbili na Timu ya Daraja la chini Plymouth, wapo kwao Anfield kucheza na Timu nyingine ya Daraja la chini Wolverhampton Wanderers. Nyingine ni huko White Hart Lane kati ya Tottenham Hotspur na Wycombe Wanderers.
Mechi ya mwisho Siku hiyo ni ile inayohusisha Timu za EPL pekee huko Saint Mary kati ya Wenyeji Southampton, ambao Juzi waliibwaga Liverpool na kutinga Fainali ya EFL CUP, dhidi ya Arsenal.
Jumapili, mbali ya Mechi ya Mabingwa Man United na Wigan, nyingine kali ni ile ya huko Selhurst Park wakati Crystal Palace wakicheza na wenzao wa EPL Man City.
EMIRATES FA CUP:
RAUNDI YA 4
Ratiba/Matokeo:
Ijumaa Januari 27
Derby County 2 Leicester City 2
Jumamosi Januari 28
1530 Liverpool v Wolverhampton Wanderers
1800 Blackburn Rovers v Blackpool
1800 Chelsea v Brentford
1800 Middlesbrough v Accrington Stanley
1800 Oxford United v Newcastle
1800 Rochdale v Huddersfield Town
1800 Lincoln City v Brighton & Hove Albion
1800 Burnley v Bristol City
1800 Tottenham Hotspur v Wycombe Wanderers
2030 Southampton v Arsenal
Jumapili Januari 29
1500 Millwall v Watford
1530 Fulham v Hull City
1700 Sutton United v Leeds United
1900 Manchester United v Wigan Athletic
1900 Crystal Palace v Manchester City

0 maoni:
Post a Comment