Saturday, January 28, 2017


MECHI za Robo Fainakli za AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zitaanza Jumamosi Januari 29 kwa Mechi 2 kati ya Burkina Faso na Tunisia na kufuatia ile ya Senegal na Cameroon.
Kati ya hizo Mechi mbili ile ya Senegal na Cameroon ndio yenye mvuto na mashamsham hasa baada ya Senegal kucheza vizuri mno kwenye Mechi zao za Kundi B kwa kuzifunga Zimbabwe na Tunisia, zote 2-0 kila moja, na kutoka 2-2 na Algeria wakati wakiwa tayari wamefuzu na pia kuchezesha Rizevu 10 wa Mechi zao 2 za awali.
Tofauti na Senegal, Cameroon, wakiwa Kundi A, walitoka Sare 1-1 na Burkina Faso, kuifunga Guinea-Bissau 2-1 na Sare na Wenyeji Gabon ya 0-0.

Lakini Kocha wa Senegal, Aliou Cisse, Mchezaji wao zamani wa Senegal, Nchi ambayo ni maarufu Kisoka kama Simba wa Teranga, amesisitiza Cameroon ni Vigogo Afrika ambao wametwaa Ubingwa wa Afrika mara 4 wakati wao hawajatwaa hata mara 1.

Ili kuondoa presha kwa Timu yake, Cisse, ambae alikuwa Nahodha wa Simba wa Teranga, amesisitiza: “Hatuwezi kuwa sisi ndio tunaotegemewa kutwaa Ubingwa wakati pia wapo Ghana, Morocco na Congo DR ambao wameonyesha ni wazuri mno!”

Robo Fainali nyingine mbili za AFCON 2017 zitachezwa Jumapili.

AFCON 2017
RATIBA
Robo Fainali

Jumamosi Januari 28
1900 Burkina Faso v Tunisia [RF 1]
2200 Senegal v Cameroon [RF 2]

Jumapili Januari 29
1900 Congo DR v Ghana [RF 3]
2200 Egypt v Morocco [RF 4]

Nusu Fainali
Jumatano Februari 1

2200 Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4

Alhamisi Februari 2
2200 Mshindi RF 2 v Mshindi RF 3

Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4

2200 Aliefungwa NF 1 v Aliefungwa NF 2

Fainali
Jumapili Februari 5

2200 Mshindi NF 1 v Mshindi NF 2

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog