Jana
Usiku huko England, Klabu nyingi za Ligi Kuu England zilifanya Hafla
maalum kutunuku Tuzo kwa Wachezaji wao Bora wa Msimu wa 2014/15 ambao
unamalizika Jumapili hii.
Huko Manchester United, Meneja wao louis
van Gaal alijizolea sifa kemkem kwa spichi yake murua iliyofurahisha na
kuhamasisha na kushangiliwa mno Ukumbini na kujizolea sifa kubwa katika
Mitandao ya Jamii.
Katika
Hafla hiyo, kwa Misimu miwili mfululizo, Kipa David De Gea alitwaa Tuzo
mbili za Mchezaji Bora wa Wachezaji, inayochaguliwa na Wachezaji
wenyewe, na ile ya Mchezaji Bora wa Washabiki, inayopigiwa Kura na
Mashabiki.
Hivi sasa Kipa De Gea amegubikwa na uvumi wa kutaka
kuhamia Real Madrid licha ya kupewa Mkataba mpya ulioboreshwa ambao
hajausaini.
Tuzo za Goli Bora la Msimu ilikwenda kwa Juan Mata kwa Goli lake la pili dhidi ya Liverpool.
Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana ilichukuliwa na Mbrazil Andreas Pereira.
Huko
Liverpool, Winga machachari, Raheem Sterling alizomewa wakati akipanda
Jukwaani kupokea Tuzo yake ya Mchezaji Bora Kijana wa Msimu.
Sterling
alipokewa kwa shangwe iliyobadilika na kuja kuzomewa na miluzi ikiwa ni
ishara ya Washabiki kuchukizwa kwa kukataa kwake kusaini Mkataba mpya
akidai kuhama Klabu hiyo.
Lakini
Mbrazil Philippe Coutinho ndie alieibuka Shujaa wa Liverpool kwa kutwaa
Tuzo 3 za Mchezaji Bora wa Msimu, Goli Bora la Msimu, lile la Shuti la
mbali dhidi ya Southampton na Tuzo ya Tukio la Uchezaji wa Ustadi.Meneja Van Gaal akwa na mshindi tuzo mara mbili David de Gea (Tuzo mbili za Mchezaji Bora wa Wachezaji)
Van Gaal, De Gea pamoja na Steve Cross wakiwa na Kombe kama Tuzo ya Sir Matt Busby mchezaji bora wa mwaka.