Friday, August 1, 2014

HOTUBA YA MWISHO WA MWEZI JULAI KUTOKA KWA RAIS JAKAYA KIKWETE Utangulizi Ndugu wananchi; Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kwa mara nyingine tena kuzungumza na taifa juu ya masuala muhimu yanayohusu nchi yetu. Mwezi wa Saba tunaoumaliza leo ulikuwa na matukio mengi baadhi yakiwa makubwa na kushtusha na mengine yalikuwa matukio...
Anaconda, Lady Jay Dee ambaye ameshinda tuzo ya AFRIMMA kama mwimbaji bora wa kike Afrika Mashariki atatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, August 3 mwaka huu akitokea Marekani. Akiongea na mwandishi, meneja wa Lady Jay Dee, Captain Gardener G. Habash amesema kuwa mwimbaji huyo anatarajia kuondoka Houston, Marekani August 1 na kuingia Dar es Salaam...
Wanaume wanaounga mkono mapenzi ya jinsia moja Uganda Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada. Kadhalika...
Rudisha alikuwa bingwa wa Olimpiki mjini London mwaka 2012 Bingwa wa Olimpiki na ambaye pia anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 mkenya David Rudisha aliambulia medali ya fedhakatika mashindano ya Jumuiya ya madola. Hii ni baada ya kushindwa na mshindani wake wa karibu Nijel Amos mwenye umri...
Warembo wakiwa kambini,katika pozi la picha ya pamoja. Shindano la Redd's Miss kagera 2014, Linatarajiwa kufanyika jumamosi ya tarehe 02/08/2014 katika ukumbi wa Lina's Club. ...
MALAGA imetangaza kumsajili kipa Guillermo Ochoa ili arithi mikoba ya Willy Caballero. Kipa huyo mwenye miaka 29, raia wa Mexico,  alikuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya Ajaccio kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita na alikuwa na ofa nyingi kufuatia kuonesha kiwango cha ajabu katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil. Ochoa...
+6 Mabingwa: Nyota vijana wa Ujerumani wakishangalia baada ya kutwaa taji kwa kuifunga Ureno bao 1-0 katika mchezo wa fainali. KIZAZI kijacho cha soka cha Ujerumani kimefuata nyayo za kaka zao kwa kushinda kombe lingine la Ulaya la vijana chini ya miaka 19. Kiungo wa Hertha Berlin, alifunga bao pekee lililowapa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ureno huko Budepest. Timu ya...
DIEGO Lopez yupo tayari kuondoka Real Madrid majira haya ya kiangazi kwasababu ya kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza. Kipa huyo mwenye miaka 32 alijiimarisha chini ya Carlo Ancelotti aliyependelea kumuanzisha katika mechi za La Liga msimu uliopita, lakini alipoteza nafasi hiyo kwa kipa mwenzake Iker Casillas aliyekuwa anapangwa zaidi katika mechi za kumalizia msimu. Kwa wiki...
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam KOCHA mkuu wa Yanga sc, Mbrazil, Marcio Maximo kesho anaweza kuwataja wachezaji atakaowatumia katika michuano ya kombe la Kagame itakayofanyika mjini Kigali, Rwanda kuanzia Agosti 8 mwaka huu. Katibu mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema Maximo atazungumza na waandishi wa habari kesho baada ya mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo...
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam KLABU ya Simba sc imemalizana na klabu ya Ruvu Shooting kuhusu kumsajili mshambuliaji wa maafande hao, Elias Maguri . Afisa habari wa klabu hiyo, Masau Bwire amesema wakati wa sikuu ya Eid El Fitri, Simba walipeleka ofa, wakakaa pamoja na kujadili na hatimaye kufikia makubaliano. “Simba wamefuata taratibu zote, wamekuja kwetu,  kwasababu Maguri ana mkataba...
JOSE Mourinho ameweka wazi kuwa kipa namba moja wa muda mrefu wa Chelsea, Petr Cech anaweza kuondoka klabuni hapo majira haya ya kiangazi mwaka huu. Baada ya Thibaut Courtois kurejea klabuni kutokea klabu ya Atletico Madrid alipokuwa anacheza kwa mkopo, tetesi zimeshaanza kuzuka kama kipa wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech ataendelea kushikilia namba moja katika dimba la Stamford Bridge. Mtandao...
UEFA imethibitisha kuwa itachunguza tatizo la mashabiki kuvamia uwanja katika mechi ya kufuzu ligi ya mabingwa barani Ulaya baina ya Copenhagen na Dnipro Dnipropetrovsk. Kipindi cha pili katika mechi  hiyo ya kwanza ya raundi ya tatu iliyopigwa uwanja Kiev Olympic ilisimama kwa dakika 10 baada ya mashabiki wageni kutoka Uholanzi kuingia uwanjani wakijihami kushambuliwa na kundi...
  SAKATA la usajili wa mshambuliaji wa Mbeya City, Saady Kipanga, kwenda Simba, limechukua sura mpya baada ya viongozi wa klabu hiyo kushindwa kuelewana kwa maelezo kwamba kigogo mmoja amemsajili kibabe bila wenzake  kuridhia. Awali viongozi wa Kamati ya Usajili kwa ushirikiano na viongozi wengine wa Simba, walikubaliana kufuta usajili wa mchezaji huyo. Lakini baadaye mmoja...

waliotembelea blog