NAHODHA
wa zamani wa Arsenal, Mfaransa Thierry Henry anaamini klabu hiyo
inapaswa kutumia kipindi kilichobaki kabla ya dirisha la usajili
kufungwa Septemba 2 kununua kiungo na mshambuliaji.
The
Gunners ililazimishwa sare ya bilakufungana na Liverpool usiku wa jana,
licha ya kutawala sana mchezo kipindi cha pili, huku kipa Petr Cech
akiokoa michomo miwili ya hatari mno ya Christian Benteke na Philippe
Coutinho kipindi cha kwanza.
Henry
anaamini timu yake hiyo ya zamani inahitaji kuongeza makali katika safu
yake ya kiungo na ushambuliaji kama wanataka kugombea ubingwa wa Ligi
Kuu ya Engand msimu huu, wazo ambalo liliungwa mkono na mchambuzi
mwenzake wa Sky Sports, Jamie Carragher.
Thierry Henry anataka Arsenal isajili kiungo mkabaji au mshambuliaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa
"Nafikiri
itakuwa wiki ya aina yake, watanunua mtu mmoja wa mbele au wa katikati
ya Uwanja? Waliwakosa wachezaji wengi usiku huu (jana),
bado wanahitaji kiungo mkabaji na bado wanahitaji mshambuliaji.
Tumekuwa tukisema hivi tangu mwanzoni mwa msimu,"amesema Henry.
Carragher
akaongeza kwamba baada ya Arsenal kushindwa kufunga bao katika mechi
zao mbili za kwanza nyumbani, hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka
1979 na sare hiyo inamaanisha timu ya Mfaransa, Arsene Wenger imeshindwa
kufunga bao katika mechi zake tano zilizopita za Ligi Kuu ya England
nyumbani.
0 maoni:
Post a Comment