Rais
wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Akizungumza katika Uzinduzi
Huo Akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani
Kajula (Kushoto) Pamoja na Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile
Solutions, Bi Lulu Ramole.
Simba
Sports Club kwa kushirikiana na Kampuni ya Tigo Tanzania zimezindua
huduma ya ujumbe mfupi ijulikanayo kama ‘SIMBA NEWS’, ambayo lengo lake
nikuwapatia wateja wa Tigo taarifa zinazoihusu klabu ya Simba popote
walipo nchini.
Huduma
hii mpya inajulikana kama ‘SIMBA NEWS’. Njia hii ni rahisi na yenye
ufanisi yenye kuifanya dunia ijulikane kwa wateja wake. “Pamoja na kasi
yaukuaji wa Tehama, Tigo inaelewa umuhimu wakutoa taarifa kwa wateja
wake, ndiyo maana leo, tunajisikia fahari kuzindua huduma hii
iliyotengenezwa vizuri ya SIMBA NEWS nawashirika wetu wa klabu ya SIMBA,
EAG Group LTD pamoja na Premier Mobile Solutions (PMS), ilikuendelea
kuwapa wateja wetu taarifa zinazohusu masuala ya sasa huku wakifurahia
habari mpya zinazohusu klabu,”alisema meneja wa mawasiliano ya
kibiashara Jacqueline Nnunduma.
Lengo
letu si tu kuwapatia wateja wetu taarifa kiurahisi zaidi, lakini pia
kuwapatia taarifa hizo kwa wakati na zenye uhakika kutoka vyanzo vya
michezo vyenye kuaminika,” aliongeza Nnunduma.
Akizungumza
kwa niaba ya Klabu ya Simba,Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva alisema,
“Tunaamini ubunifu huu bila shaka utawawezesha mashabiki wote wa Simba
na wa soka kwa ujumla ambao pia ni wateja wa Tigo kupata habari
mbalimbali za klabu ya Simba kupitia simu zao za mkononi”.
Tunawahimiza
mashabiki wetu kujiunga na huduma hii kupitia Tigo ili waweze kupata
nakufurahia habari mbalimbali kutoka klabu ya Simba. Aliendelea Aveva.
Akiongea
katika tukio hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani
Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa shughuli za kibiashara na
masoko katika klabu ya Simba, alisema “Tunatarajia kuendelea kuwapatia
mashabiki wa Simba huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia zisizokuwa na
usumbufu wa aina yeyote kupitia wadau wanaoaminika ndani ya Tanzania”
Kwa
upande wake Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu
Ramole alisema kuwa huduma hii imetengenezwa ili kuwawezesha wateja
kupata habari za papo kwa papo naaliongeza kuwa huduma ipo katika mfumo
wa vifurushi vya Combo / BUNDLE PACK ambapo wateja wa Tigo watakuwa
wakilipia mara moja kwa siku na kupokea kiwango cha chini cha habari nne
(04) na habari mpya za kila siku zina zohusu klabu ya Simba.
Huduma
pia itamruhusu mteja aliyejiunga kujitoa kwenye huduma hii wakati
wowote akitaka bila vikwazo vyovyote na pia kwenye huduma hii kutakuwepo
na neon kuu “MSAADA”kwa ajili ya kusaidia juu ya maswali mbalimbali ya
nayo ulizwa mara kwa mara na wateja wakati wakifurahia huduma.
Ili
kujiunga na huduma hizi unatakiwa kutuma neon kuu SIMBA kwenda 15460.
Utakapo jiunga tu mteja atapokea habari kutokana na neon analolituma
kila siku na atatozwa kiasi cha shilingi za kitanzania 150 kwa siku. Na
ili kujitoa kwenye huduma mteja atahitaji kutuma neno ONDOA SIMBA kwenda
15,460.
0 maoni:
Post a Comment