John Bocco akishangila baada ya kuipatia Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati .
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager imetoka sare
ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The Cranes) katika mchezo wa
kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017 nchini Rwanda uliofanyika
uwanja wa Nakivubo.
Stars ambayo leo imeonekana
kabadilika katika mchezo wa leo, ilicheza soka la kuvutia tangu mwanzo
mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaduwaza wenyeji Uganda.
Mpaka dakika 45 za mchezo za
kipindi cha kwanza zinamalizika, Uganda 0 – 0 Tanzania. Kipindi cha pili
kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi mfululizo kupitia kwa
washambuliaji wake John bocco na Rashid Mandawa.
Dakika ya 58, John Bocco aliipatia
Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa Uganda
Bakaki Shafik kuunawa mpira wa ndani ya eneo la hatari.
Mara baada ya bao hilo Uganda
walifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Stars na kufanikiwa kupata
bao la kusawzisha dakika ya 82, kupitia kwa mchezaji Kizito Hezron.
Mashabiki.
Mpaka dakika 90 za mchezo
zinamalizika Uganda 1 – 1 Tanzania. Kwa matokeo hayo Uganda wanasonga
mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 – 1 na sasa watakutana na Sudan.
Mara baada ya mchezo huo kochaa
mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema anashukuru vijana wake
wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo ulikua mzuri timu ilitengeneza
nafasi chache na kuweza kutumia nafasi moja iliyopatikana.
Mkwasa amewaomba watanzania
kuendelea kuwapa sapoti, wamekaa na timu kwa muda mfupi wa wiki moja tu
lakini katika mchezo wa leo mabadiliko yameonekana, hivyo wanahitaji
muda kidogo kuweza kukaa na vijana kwa muda mrefu ili kujenga timu bora.
Rashid Mandawa akimtoka Hassani Maswa.
Stars inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda Air.
Taifa Stars: Ally Mustafa, Shomari
Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mudathir Yahya,
Deus Kaseke, Frank Domayo,/Said Ndemla John Bocco, Rashid Mandawa/Salum
Telela, Saimon Msuva/Ramadhan Singano.
The Cranes: James Alitho, Muzamiru
Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan Waswa, Denis Oola, Faruk Miya, John
Shemazi/Robert Sentongo, Bakaki Shafik, Tekkwo Derick/Kizito
Hezron/Kalanda Frank.
Kikosi cha Taifa Stars.
0 maoni:
Post a Comment