Ofisa
Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei
(katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom
Tanzania lililopo katika maduka ya Shoppers plaza Mbezi Beach jijini Dar
es Salaam.Wengine katika picha kushoto ni mteja wa kwanza kufika kupata
huduma katika duka hilo Bw.Argylle Tsvakai na Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.
Mteja
wa kwanza kufika katika duka jipya la Vodacom Tanzania Bw.Argylle
Tsvakai (kulia) akiangalia moja ya simu zinazouzwa kwa bei nafuu katika
duka hilo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini
Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa rasmi na Afisa Mkuu wa Idara ya Mauzo
na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei (kushoto). Katikati ni
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn
Mworia.
Ofisa
Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei
(kushoto) akimmiminia mvinyo kwenye glasi Bw.Argylle Tsvakai ambaye
alikuwa ni mteja wa kwanza kufika kupata huduma katika duka jipya la
kampuni hiyo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach
jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa rasmi leo. Anayeshuhudia
katikati ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,
Rosalynn Mworia.
Baadhi
ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimfanyia
mahojiano Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom
Tanzania, Rosalynn Mworia baada ya kuzinduliwa kwa duka jipya la kampuni
hiyo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es
Salaam.
Picha
ya pamoja ya baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wadau wao
walioshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo leo lililopo
katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
KATIKA
kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Mbezi Beach na maeneo jirani ya
Tegeta, Kawe na Boko wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano
ya Vodacom leo imefungua duka jipya la kisasa katika eneo la Mbezi
Beach kwenye maduka ya Shoppers Plaza.
Mbezi
Beach ni moja ya kitongoji maarufu katika jiji la Dar es Salaam ambacho
kinakua kwa kasi kwa maendeleo na kuwa kivutio cha wawekezaji wengi
kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu na shughuli mbalimbali za
kibiashara ikiwemo maofisi,mahoteli pia ni njia kuu ya kuelekea katika
mji wa kihistoria wa Bagamoyo.
Duka
hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma
mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma kwa mawakala wa M-pesa
na uuzaji wa bidhaa mbalimbali za Vodacom na litawawezesha wateja wa
Mbezi Beach na vitongoji vyake wakiwemo wasafiri wanaoelekea na
kutokea Bagamoyo na wateja kutoka maeneo ya Kawe,Tegeta, Goba na Mbezi
juu.
Mtandao wa Vodacom unaongoza kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika wilaya ya Kinondoni.
Mkuu
wa kitengo cha Uhusiano na Mawasliano wa Vodacom Tanzania, Rosalyn
Mworia, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa ni mwendelezo wa
malengo ya Vodacom kuendeleza kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania
kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa
urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya za kilimo klabu
na M-Pawa zinazolenga kuwawezesha kuwawezesha wananchi na kuwarahishia
maisha.
“Uzoefu
na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao
unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya
juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya
wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua
maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na
ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na
tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha
ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora
kwa gharama nafuu.”Alisema Mworia.
Naye
Mkazi wa Mbezi beach na Mteja wa kwanza kupata huduma katika duka hilo
baada ya kuzinduliwa duka hilo aliipongeza hatua ya kusogezewa huduma
karibu “Tunapongeza jitihada za kampuni hii inazozifanya katika
kuwasogezea wateja wao huduma za mawasiliano karibu na makazi yetu kwani
itatuwia rahisi kupata huduma kwa karibu badala ya kwenda mbali na huu
ni uthibitisho kuwa hivi sasa jiji la Dar es Salaam linazidi kupanuka na
huduma kuwafuata wananchi kwa karibu”.Alisema Bw.Argylle Tsvakai mkazi wa Mbezi Beach.
Vodacom
ina mtandao wa maduka 87 na wakala mbalimbali wa kuuza bidhaa zake
nchini na duka lililofunguliwa leo ni la 88 kufunguliwa katika wilaya
ya Kinondoni.
0 maoni:
Post a Comment