Kaimu
Mku wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, BGML,
Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya
Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima kirefu cha maji
kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko Bugarama. BGML, inayomilikiwa
na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi mine ya elimu na maji kwa Halmashauri
hiyo yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni
Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto),
akiongozana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala
Mkoani Shinyanga, Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Busindi, Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za
walimu, zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na
kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri ya
wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi Bilioni 1,
kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015.
MOJA
kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na
mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani
Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, umekabidhi
miradi minne ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa
ni sera ya kampuni kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi.
NA
K-VIS MEDIA
MGODI
wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, Jumatatu Agosti 31, 2015, umekabidhi miradi,
yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwa Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya
Msalala mkoani Shinyanga.
Akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi huo unaomilikiwa na
Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Michell Ash, alisema, “Sisi BGML tulitoa
ufadhili wa kugharimia miradi ya kijamii kwa wenyeji wetu na leo tunakabidhi
miradi hiyo minne baada ya kukamilika kwake ikiwa ni ishara ya muendelezo wa
utekelezaji wa ahadi zetu za kampuni kuwajibika kusaidia jamii.” Alisema.
“Ninayo
furaha kuu kutangaza kuwa BGML ilifadhili miradi minne kwa thamani ya shilingi
bilioni 1,100,546,766 na tunatarajia kutoa fedha zaidi mwaka huu kusaidia sekta
za Afya na Elimu.”Alifafanua.
Akitoa
mchanganuo wa miradi iliyogharimiwa na mgodi huo ulioko wilayani Msalala, Ash
alisema, BGML ilikamilisha ujenzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya msingi
Bugarama kwa thamani ya shilingi milioni 403,437,000, kukamilisha ujenzi wa
madarasa sita na na ujenzi wa tenki la maji kwenye shule ya msingi Busindi kwa
thamani ya shilingi 129,333,860 na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba mbili za
walimu na ofisi ya walimu shule ya msingi Busindi kwa gharama ya shilingi 137,229,200.
Miradi
mingine ni Ujenzi wa visima sita vya maji huko Kakola(1) na Kakola (9),
Buyange, Bushing’we, shule ya sekondari Bugarama, Mwasabuka yote ikiwa na
gharama ya shilingi 174,392,000.
Hali
kadhalika BGML ilikamilisha ujenzi wa maabara ya Biolojia, Kemia na Fizikia
kwenye shule ya msingi Nyikoboko ikitumia kiasi cha shilingi 256,154,706.
Akitoa
shukrani za wilaya baada ya kupokea miradi hiyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya
Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema, ni
faraja ilioje kuona wawekezaji wanaonyesha moyo wankuisaidia jamii inayozunguka
mgodi huo.
“Nataka
niseme, mafanikio haya tunayoyaona leo hii ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati
ya wananchi na wawekezaji, ambapo wameamua kusaidia pale wananchi wanapokwama.”
Alisema na kutoa wito kwa uongozi wa shule na maeneo yaliyokabidhiwa miradi
hiyo kuitunza.
Kukabidhiwa
kwa miradi hiyo ni utekelezaji wa Sera ya kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi
huo ya mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi yake.
0 maoni:
Post a Comment