Tuesday, September 1, 2015


Klabu ya Chelsea ya Uingereza imeonyesha muonekano wa uwanja wao mpya ambao hadi mwaka 2020 inaripotiwa ujenzi wa uwanja huo utakuwa umekamilika. Bado mashauriano yanaendelea kuhusiana na wakazi wa eneo husika utakapo jengwa uwanja huo.
2BDA18B000000578-0-image-a-4_1441054162717
Mpango wa mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich ni kutumia pound milioni 500 katika ujenzi wa uwanja huo ili uwe biashara tofauti inayojitegemea mbali na Chelsea. Ujenzi huo ambao unatarajiwa kuanza baada ya miezi 9 kutokea sasa utaifanya klabu ya Chelsea kuhama uwanja wao wa Stamford Bridge na kutumia Uwanja wa Wembley kwa kipindi cha misimu mitatu.
2BDA1DDF00000578-3217477-image-a-1_1441068450794
Ujenzi huo wa Uwanja mpya wa Stamford Bridge utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 sawa na uwanja wa Taifa wa Dar Es Salaam, ambapo uwanja wa sasa wa Chelsea unachukua watu wasio zidi 41,000.
2BDA18F000000578-0-image-a-1_1441054152161
2BDA13FB00000578-0-image-a-5_1441054173682
2BDA190700000578-0-image-a-2_1441054154803
 
Huu ni muonekano wa sasa wa Uwanja wa Stamford Bridge

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog