Monday, August 18, 2014


Manchester United wanajiandaa kuwekeza kitita cha kutosha ili kuinasa saini ya Angel Di Maria kutoka Real Madrid. 
MASHETANI wekundu, Manchester United wanajiandaa kumwaga paundi milioni 100 kumshawishi Angel di Maria kutua Old Trafford wakati huu klabu inahitaji kujiboresha ili kushindania ubingwa wa ligi kuu England.
Kocha mkuu wa United, Louis Van Gaal anahitaji kusajili wachezaji wa kiwango cha dunia kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani ulaya na tayari ameshaonja machungu ya kufungwa ambapo alilala mabao 2-1 dhidi ya Swansea jumamosi iliyopita uwanjani Old Trafford.
Mkurugenzi mkuu wa United, Ed Woodward amemuunga mkono Van Gaal na yupo tayari kufanya lolote lile ili mradi Di Maria atue Man United.
Inafahamika kuwa United imemuambia Muargentina huyo kwamba kwa kiwango chake cha sasa itamlipa mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki.
Kwa mkataba wa miaka mitano anaotarajiwa kupewa, United itawezekeza paundi milioni 100 ikijumuisha mshahara wake na ada ya uhamisho.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog