Monday, August 18, 2014


LOUIS VAN GAAL ameambiwa ni lazima aende Sokoni kusaka Wachezaji Wanne wazuri kabla Dirisha la Uhamisho halijafungwa hapo Septemba Mosi.
Huo ndio msimamo wa Kocha wa zamani wa Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson, Mholanzi Rene Meulensteen, ambae ametoboa Kikosi cha sasa si imara katika mbio za Ubingwa.
Jumamosi Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya kwanza kabisa ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England, Man United ilichapwa Bao 2-1 na Swansea City, Gemu ambayo pia ilikuwa ya kwanza kabisa ya Ligi kwa Meneja mpya Van Gaal.

Akihojiwa na Wanahabari kwenye Kipindi Maalum cha TV, Meulensteen alisema Timu hiyo inahitajika kujengwa upya.
Ameonya: “Hamna njia fupi. Bado wana Wiki mbili na lazima waende Sokoni kununua Wachezaji kwenye Kipindi hiki na kijacho cha Uhamisho cha Januari!”

Kocha huyo mahiri ambae mafanikio makubwa ya Man United yanasemwa ni mchango wake mkubwa ameongeza: “Tunahitaji kuimarisha Difensi, lazima tuongeza nguvu Kiungo na hayo ndio maeneo makubwa yanayotakiwa kutazamwa kwanza na haraka. Kwa maoni yangu, wanahitajika Wachezaji Wanne wa kiwango cha juu!”Kuhusu Van Gaal kutumia Mfumo mpya wa 3-5-2, Meulensteen ameeleza: “3-5-2 inaweza kufanya kazi. Mfumo wowote unawezekana ukiwa na Wachezaji sahihi na Wachezaji wakauelewa Mfumo huo. Ni mtirirko wa muda mrefu na walianza vizuri kwenye Mechi za kujipima kabla Msimu kuanza. Itachukua muda hadi wafikie kile kiwango cha ile Man United inayotawala, inayocheza

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog