Monday, August 18, 2014


Klabu ya Arsenal itajielekeza nchini Uturuki jumanne wiki hii kuchuana na klabu ya Besiktas katika michuano ya ligi ya mabingwa. Besiktas haijawahi kucheza na Arsenal barani Ulaya.
Mechi zingine zitakazochezwa jumanne wiki hii katika mzunguko wa kwanza ni pamoja na FC Copenhague kumenyana na Bayer Leverkusen, huku Naples ikiwa na kazi kubwa dhidi ya Athletic Bilbao.
Mwaka jana Arsenal iliishinda Fenerbahçe kwa mabao (3-0) na (2-0) katika mchuano wa marudio. Arsenal imekua ikishinda katika viwanja vya Uturuki. Klabu hiyo haijafungwa katika michuano 7 iliyocheza nchini Uturuki, huku ikifungwa mabao mawili dhidi ya mabao 12 iliyofunga timu za taifa hilo.

Arsenal ikichezea nyumbani ilishindwa kufanya vizuri juzi Jumamosi dhidi ya Crystal Palace na kulazimika kwenda sare ya kufungana bao moja kwa moja, baada ya kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya 90 ya mchezo.

Wenger huenda akafanya mabadiliko katika klabu yake baada ya kumkosa kwa muda mrefu Walcott. Monreal huenda akacheza upande wa kushoto wa ulinzi. Naye Giroud huenda akawekwa mbele kwenye nafasi ya Sanogo.

Mechi hizo za mzunguko wa kwanza zitachezwa jumanne na jumatano wiki hii. Mechi za marudio zimepangwa kuchezwa jumanne na jumatano wiki kesho.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog