Monday, August 18, 2014


Mechi ya kugombea Gamper Trophy dhidi ya Club Leon ya Mexico, Barcelona wameichakaza timu hiyo bila huruma ambapo Magoli ya Barva yamefungwa na Lionel Messi bao la mapema dakika ya 3  aliyefuata kufunga ni kijana matata Neymar aliyetokea kwenye kujiuguza majeraha yake dakika ya 12 na dakika ya 44 akifunga bao mbili.
Bao la tatu lilifungwa kipindi cha pili dakika 55 na Munir El Haddadi  na akiongeza tena bao lake la pili katika dakika ya 78.
Dakika ya 86 aliyemalizia bao ni Sandro Ramírez hivyo Mtanange kumalizika kwa bao 6-0 Club Leon wakimaliza mchezo huo bila hata bao la kufutia machozi!!!

Suarez ametambulishwa leo mbele ya mashabiki wa Barca ambapo pia wamecheza mechi ya kirafiki na kushinda bao 6-0

Suarez akisalinia Mashabiki wa Barca leo walipokuwa wakijiandaa kucheza na timu ya Mexico Club  Leon

Mambo safi!!! Luis Suarez ametambulishwa Rasmi leo jumatatu mbele ya Mashabiki wa Barcelona

Suarez (wa tatu kulia) wakiwa mbele ya Mashabiki wao leo

Suarez akiwapungia mkono Mashabiki
Majembe mapya!!! Thomas Vermaelen na Suarez katikati wakipata picha mbele ya Mashabiki wao leo huko Nou Camp.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog