Kikosi cha Arsenal kilichoanza
Kikosi cha Bayern Munich kilichoanza
Minong'ono
imeanza kuwa Robben alimtemea mate Sagna kama inavyoonekana kwenye
kiduara cha njano kwenye picha. Lakini baadhi ya watu wamesema ni jasho
lililokuwa linadondoka kutoka kwenye kidevu cha Robben.
Mkwaju huo umedakwa kwa kupanguliwa nje na kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer uliopigwa na Mesut Ozil katika dakika ya 8. Dakika ya 37 kipindi cha kwanza kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny anatolewa nje kwa kupewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia ndivyo sivyo Robben ndani ya eneo hatari, Mkwaju wa penati unatengwa. David Alaba anakosa penati mpira unagonga posti na kutoka nje!! Arsenal wanafanya mabadiliko Santi Cazorla anatoka na nafasi yake inachukuliwa na kipa Lukasz Fabianski katika dakika ya 39 kipindi cha kwanza na dakika ya 31 pia Arsenal walifanya mabadiliko ya Kieran Gibbs baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Monreal. Kosa kosa hizo za penati katika timu zote mbili zimesababisha timu zote kwenda mapumziko 0-0.
Mkwaju wa Ozil ukidakwa na kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer mapema kipindi cha kwanza!
Kipindi cha pili dakika ya 46 Bayern Munich wanafanya mabadiliko ya Jerome Boateng na nafasi yake
kuchukuliwa na Rafinha. Dakika ya 54 kipindi cha pili Toni Kroos akaifungia bao timu yake Bayern Munich baada ya kupewa pasi na Philipp Lahm.
Baadae kidogo Yaya Sanogo akapewa kadi ya njano baada ya kumchezea ndivyo sivyo kipa wa Bayern Munich Never. Dakika za
lala salama dakika ya 88 mchezaji wa Bayern Munich Thomas Müller aliyetokea benchi akaifungia bao timu yake, Bao la kichwa baada ya kupewa pasi safi na Philipp Lahm.
Kipa Szczesny akiruka na Arjen Robben...
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Wilshere, Oxlade Chamberlain, Ozil, Cazorla, Sanogo. Subs: Fabianski, Rosicky, Podolski, Giroud, Monreal, Jenkinson, Gnabry.
Bayern Munich: Neuer, Lahm, Boateng, Dante, Alaba, Thiago, Javi Martinez, Robben, Kroos, Gotze, Mandzukic. Subs: Starke, Van Buyten, Rafinha, Pizarro, Muller, Contento, Schweinsteiger.

Mwamuzi:Nicola Rizzoli (Italy)
0 maoni:
Post a Comment