RAIS wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, amefunga kozi
ya makocha lesseni C inayotambuliwa na Shirikisho la soka barani Afrika
(CAF) na kuwataka wahitimu hao kufanyia kazi mafunzo waliyoyapata.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kufunga mafunzo hayo, Malinzi amesema kuwa anasikitika kuona makocha wanapata mafunzo kama hayo lakini wanaenda kuweka vyeti vyao ‘makabatini’ na kuacha kufanyia kazi walichojifunza.
“Hiki mlichokipata kwenye mafunzo haya ya wiki mbili mnatakiwa muende mkafanyie kazi kwa kutafuta timu za kufundisha na baada ya mwaka mmoja ni vizuri mkajiendeleza zaidi ya hapa,” alisema Malinzi
Aidha, amesema kuwa Shirikisho lake limepanga kuhakikisha baada ya muda litafuta utaratibu wa makocha wenye lesseni C kuwa kwenye benchi la ufundi la timu za daraja la kwanza na kuwa wasaidizi kwenye benchi la ufundi la timu za ligi kuu.
“kwa sasa hivi makocha wa ligi kuu wanatakiwa kuwa na leseni ya daraja B na wasaidizi angalau leseni daraja C, ila kuanzia msimu wa 2017-2018 mambo yatabadilika na lessen I C aizataruhusiwa kwenye mabenchi ya ufunzi kwa timu za ligi kuu, mambo yataendelea hivyo mpaka mwisho tutakuwa na leseni za daraja A,” alisema Malinzi.

0 maoni:
Post a Comment